October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia aomba sekta binafsi kumuunga mkono matumizi ya fedha za IMF

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

Rais SAMIA Suluhu Hassan ameomba sekta binafsi kumuunga mkono kwa kuchangamkia fursa zinazotokana na fedha zilizotolewa na Shirika la Fedha Duniani (IMF) zitakazotumika kutekeleza miradi ya maendeleo na kuboresha huduma za jamii kama vile maji, afya elimu. Anaripoti Mwandishi wetu… (endelea)

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 10 Oktoba, 2021 jijini Dodoma wakati akizindua mpango wa kampeni ya maendeleo kwa ustawi na mapambano ya UVIKO -19 ambao umetokana na mkopo nafuu wa Sh trilioni 1.3 uliotolewa na Shirika hilo la IMF.

Ametoa wito kwa sekta binafsi kuchangamkia fursa kwa kuzalisha bidhaa ambazo zitakazotumika kwenye utekelezaji wa miradi hiyo kama vile saruji na mabati.

“Kuna madarasa 15,000 na vituo vya afya zaidi ya 200 vinakwenda kujengwa na kufanyiwa ukarabati. Tunaomba sekta binafsi wachangamke na kutuunga mkono ili tusiwe na sababu ya kuchelewa kutumia pesa hizi.

“Fedha hizi ni za miezi tisa tu, kwa hiyo niombe wajitahidi kutuunga mkono,” amesema.

error: Content is protected !!