October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia: Tunashukuru IMF, tumejadiliana wakatuelewa

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan amelishuruku Shirika la Fedha Duniani (IMF) kwa kuielewa Serikali ya Tanzania na kuridhia itumie fedha za maendeleo kwa ustawi na mapambano ya UVIKO -19 kwa namna inatakavyoona inafaa. Anaripoti Mwandishi wetu (endelea)

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 10 Oktoba, 2021 jijini Dodoma wakati akizindua kampeni ya maendeleo kwa ustawi na mapambano ya UVIKO -19 ambao umetokana na mkopo nafuu wa Sh trilioni 1.3 uliotolewa na Shirika hilo la IMF.

Amesema mpango uliozinduliwa leo utagharimu fedha nyingi katika miradi mbalimbali itakayotekelezwa kwa nchi nzima yaani Tanzania Bara na Zanzibar.

Amesema upatikanaji wa fedha ulikuwa na ‘mbinumbinu’, lakini anashukuru IMF kwa kuelewana  na Serikali ya Tanzania na kujadiliana kisha wakaleta timu yao ya watalaam ambayo iliendelea kujadiliana na Tanzania.

“Wenzetu waliopata pesa hizi wamezielekeza mzigo wote kwenye manunuzi ya chanjo na vitu vingine vya kujikinga na Corona, kwa upande wetu tukasema hapana.

“Ili tuweze kukabiliana vema na Corona lazima tuwe na maji, tupunguze masafa ya wanafunzi kubana, lazima tuwe vituo vya afya vingi vitakavyotoa huduma zipasavyo kuanzia ngazi ya wilaya hadi chini ili Corona ikipiga hadi kule chini kuwepo na vituo vya afya. Tunashukuru walituelewa wakaridhia fedha hizi tuzitumie kama sisi tulivyoona inafaa.

error: Content is protected !!