October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Majaliwa: Rais Samia utaupita 2025 na kumaliza vizuri 2030

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Spread the love

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuahidi Rais Samia Suluhu Hassan kuwa atauvuka vizuri mwaka 2025 na kuumaliza mwaka 2030 kutokana na kazi nzuri anayoifanya ya kuiongoza Serikali ya awamu ya sita. Anaripoti Mwandishi wetu (endelea…)

Majaliwa ametoa ahadi hiyo leo tarehe 10 Oktoba mwaka huu katika azinduzi kampeni ya maendeleo kwa ustawi na mapambano ya UVIKO -19 ambao umetokana na mkopo nafuu wa Sh trilioni 1.3 uliotolewa na Shirika la Fedha Duniani (IMF).

Mapema Septemba 8 mwaka huu IMF ilitangaza kutoa mkopo wa dharura wa dola za Marekani milioni 567.25 (trilioni 1.3) kwa Tanzania kwa ajili ya kukabiliana na janga la virusi vya corona, kama vile kufufua uchumi ulioporomoka.

Majaliwa amemuahidi Rais Samia kuwa atasimamia ipasavyo kazi anayoifanya kwa kuwa hata Watanzania wameona kazi nzuri anayoifanya.

“Watanzania wameiona tuna matumaini makubwa na tutaendelea kuhakikisha malengo yako yanafika mpaka vijijini, umeanza vizuri, unaendelea vizuri, utaupita vizuri zaidi mwaka 2025, na utamaliza vizuri 3020, Samia oyee!, Mwinyi oyee!” alisema Majaliwa.

Aidha, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba amefafanua kwa kina namna fedha hizo zitatumika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwamo kwenda kununua mashine 85 za kidijitali za X-Ray

“Tunakwenda kununua CT scan mashine 29 kwa mpigo kwenye hospitali za mikoa yote ili watu wetu sasa wasihangaike kufuata huduma hii kwenye hospitali chache.

“Tunaongeza ICU 72 kwa mpigo katika kila hospitali za rufaa za mikoa na baadhi ya wilaya kutoka 5 zilizokuwepo maeneo hayo kwa ajili ya kunusuru maisha ya watanzania ambao wanakuwa wanahitaji huduma hiyo.

“Tunakwenda kujenga madarasa 15,000 kwa mpigo kwenye shule zetu za sekondari. Tunakwenda kujenga madarasa 3,000 kwenye shule shikizi za msingi. Tunaenda kununua madawati 462,795 ili kuondoa mbanano wa watoto madarasani,” alisema.

error: Content is protected !!