Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari Magufuli aomba wimbo wa Prof Jay, acheza
Habari

Magufuli aomba wimbo wa Prof Jay, acheza

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, John Magufuli ameonesha kufurahishwa na wimbo ya Joseph Haule maarufu Profesa Jay, na kutaka upigwe ili asikilize na kutazama. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Ametoa ombi hilo leo Alhamisi tarehe 25 Februari 2021, alipokwenda kuzindua Jengo la Jitegemee lenye Studio za African Media ambayo ni Kampuni tanzu ya Uhuru Media, jijini Dar es Salaam.

Kampuni hiyo inabeba vituo vya Channel ten, Channel ten Plus, Magic FM na Classic FM. Baada ya kuzindua studio hiyo, Rais Magufuli aliuliza maswali kadhaa na kisha aliuliza ‘muziki unapigwa wapi?”

Alielezwa kwamba, kuna vyumba viwili (studio na control room – chumba cha kuongoza matangazo) ambavyo huwasiliana, na ndipo alipoomba apigiwe muziki wa Prof. Jay.

“Nipigie ule muziki wa Profesa Jay unaitwa.. unaitwaaa.. Naongea na Wewe,” sekunde chache muziki huo ukaanza kupigwa.

https://www.youtube.com/watch?v=0kdqo_o9jIQ

Rais Magufuli alitumia zaidi ya dakika moja kuutazama huku akicheza na kuonesha tabasamu la kuufurahia, kisha akasema “huu wimbo una ujumbe.”

Wimbo huo, unaitwa ‘Baba,’ umetolewa Januari 2021 ambao umeibwa na Stamina akimshirikisha Profesa Jay.

Profesa Jay amewahi kuwa Mbunge wa Mikumi mkoani Morogoro kati ya mwaka 2015-2020, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kabla ya kufika kwenye studio hizo, Rais Magufuli alizindua jengo hilo la CCM ambapo alisema, kwa miaka 16 lilikuwa limetelekezwa huku aliagiza lifanyiwe ukarabati ambapo sasa linatumika kutoa ajira kwa Watanzania kwa kuwa, linatumika.

“Vyombo hivi vilikuwa vya CCM lakini katikati hapa vilichukuliwa na watu, tulinyang’anywa vikachukuliwa, nampongeza Dk. Bashiru (Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu CCM) akagundua hili, tukarejesha CCM. Mnaweza kuona ufisadi ulivyoota mizizi mpaka kwenye vyombo vya CCM vilichukuliwa,” amesema.

Awali, Rais Magufuli alianza ziara yake ya siku ya pili aliyoanzia jana kwa kuweka Jiwe la Msingi katika ujenzi wa Soko Kuu la Kisutu.

Soko hilo ambalo lipo kwenye ujenzi, imeelezwa kuwa na ghorofa nne kwenda juu na chini zaidi kukiwa ni sehemu ya kuegesa magari.

Baada ya sehemu yakuegesha magari, sakafu inayofuata itakuwa na machinjio ya kuku na wafanyabiashara wadogowadogo na kisha sakafu ya kwanza juu na ya nne itakuwa ya maduka pamoja na mabucha na zingine zitakuwa na huduma zingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!