Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Madiwani wakwapuaji waahidiwa kibano
Habari za Siasa

Madiwani wakwapuaji waahidiwa kibano

Spread the love

 

MAKAMU wa Rais Tanzania, Samia Suluhu Hassani amewaonya tabia ya madiwani kutumia fedha za mifuko ya kuwezesha wananchi kwa ajili ya masilahi yao binafsi ya kisiasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tanga … (endelea).

Mama Samia metoa kauli hiyo leo Jumatano, tarehe 17 Machi 2021, katika viwanja vya Tangamano, Tanga Mjini, ikiwa ni siku ya tatu kati ya tano ya ziara yake mkoani humo.

Amesema, diwani yeyote atakayebainika kutumia vibaya fedha hizo, atachukuliwa hatua.

“Wito wangu, mfuko huu sasa usitumike kama mfuko wa kisiasa kwa madiwani.”

“Ndugu zangu madiwani, mfuko huu mlikuwa mmeugeuza kujijenga kisiasa. kila mtu anavutia kwake, tumewafumbia macho kipindi hiki, kipindi kijacho nasimama na nyie,” amesema Mama Samia.

Ametoa onyo hilo baada ya kubaini upotevu wa fedha za mifuko ya uwezeshaji wananchi, ambapo inadaiwa baadhi ya madiwani wakati wa kampeni za uchaguzi huzitumia kuwapa wananchi ili kuwashawishi wawachague, kisha hazirudishwi.

“Kama mwaka huo umevuna Sh. 100 Mil zitakwenda kwa vikundi 50, kila kikundi mtapata 2 Mil. ukichukua hapo kila kikundi kuna watu watano, pesa hizo wanakwenda kugawana. Mikopo kwenye mifuko hairudishwi wanajua diwani wetu katupa, ukija uchaguzi mambo yake yameyea,” amesema Mama Samia.

Mama Samia ameshauri fedha hizo zigawiwe kwa vikundi vichache vitakavyoweza kuzifanyia kazi ili zirudishwe na kutolewa kwa wengine.

“Mifuko hii ni mimi na wewe, kuwepo tena itakuja kutokana na ufanisi wa mfuko huu, ni vyema kutoa kwa vikundi vichache vinavyotambulika wakafanya kazi wakarudisha pesa ikaenda katika vikundi vingine. Kuliko kila diwani apate haijulikani zimeenda wapi,” amesema Mama Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!