May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Aweso aonya mamlaka za maji

Juma Aweso, Waziri wa Maji

Spread the love

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso ameonya tabia ya watumishi wa mamlaka za maji kuwabambikia bili za maji wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tanga … (endelea).

Onyo hilo amelitoa leo Jumatano tarehe 17 Machi 2021, katika ziara ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassani mkoani Tanga, iliyofanyika kwenye viwanja vya Tangamano, Tanga Mjini.

Aweso amesema, hatomfumbia macho mtumishi yeyote atakayewapandishia bili wananchi kinyume cha sheria.

“Ni haki ya wananchi kupatiwa huduma ya maji, lakini asisahau ana wajibu kulipia bili za maji. Pamoja na kulipia bili ya maji, isiwe bambikizi, leo mtu anatumia maji ya Sh.20,000 unamwambia alipe 160,000 kama ana kiwanda, haiwezekani.”

“Kelele hizi za bili za maji iwe ni mwanzo na mwisho kuzusikia, wembe ni ulele, atakayezingua nitamzingua mchana kweupe,” amesema Aweso.

Waziri huyo wa maji, amewaagiza wasoma mita za maji wote nchini, kulitekeleza jukumu hilo kwa kuwahsirikisha wananchi, ili kukwepa vitendo vya udanganyifu.

“Anapokuja msoma mita kusoma bili za maji, naomba niwalekeze wasoma mita wawashirikishe wananchi, na wasipowashirikisha si busara kuwazidishia wananchi bili za maji,” amesisitiza Aweso.

error: Content is protected !!