May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mama Samia: CCM iisaidie serikali

Spread the love

MAKAMU wa Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassani amekitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM), kusaidia serikali katika utekelezaji wa majukumu yake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tanga … (endelea).

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano tarehe 17 Machi 2021, katika ziara yake ya siku tano mkoani Tanga, iliyoanza Jumatatu na kutarajiwa kufika tamati Ijumaa ya tarehe 19 Machi 2021.

Mama Samia amesema, serikali ina jukumu la kutafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, hivyo viongozi na wanachama wa chama hicho katika ngazi za chini, wanatakiwa kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa ilani hiyo.

“Nilivyokuwa Pangani nilisema na leo nirudie hapa, halmashauari hizi zisimamiwe na CCM, ninyi mlitupa ilani ya serikali tutekeleze, na asilimia kubwa itatekelezwa na halmashauri zetu.”

Halmashauri zikizubaa, huku chini sisi tulioko Dodoma hatuzioni, jicho letu huku chini ni ninyi CCM.

“Sisi serikali tunakwenda mbio kutafuta fedha za kutekeleza mliyotutuma, usimamizi wote uko chini yenu. Nitafurahi sana nikisikia kila muda CCM wilaya furani inazunguka kuangalia miradi inayotekelezwa kuona utekelezwaji wake,” amesema Mama Samia.

Pia, ametoa wito kwa viongozi wa CCM na wanachama wake kuanika halmashauri zinazoshindwa kutekeleza ilani hiyo, ikiwemo kutotoa huduma stahiki kwa wananchi.

“Ninyi mnaweza kutuambia  halmashauri kadhaa haifanyi vizuri au katika halmashauri hii idara hii haifanyi vizuri, mkitupatia taarifa sisi tutaweza kuchukua hatua za haraka, niwaombe sana ndugu zangu wa CCM. Tusaidiane katika  kutekeleza ilani yetu,” amesema Mama Samia.

error: Content is protected !!