October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Machinga Complex sasa kujengwa kila wilaya

Machinga Complex

Spread the love

KASSIM Majaliwa Waziri Mkuu amesema ili kumaliza tatizo la ukosefu wa ajira, masoko ya wafanyabiashara ndogondogo kama Machinga Complex yanatakiwa kujengwa katika halmashauri zote nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Waziri Mkuu ameyasema alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema bungeni leo tarehe 12 Mei 2020, kwamba Machinga Complex haionekani kuwa suluhu ya matatizo ya ajira.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa soko kama la Machinga Complex ni muhimu likawa kwenye halmashauri zote nchini sambamba na kuboresha miundombinu ya umeme, maji, barabra, pamoja na majengo.

Wakati huo huo, Lema pia ameuliza swali lingine, lini serikali itapeleka fedha kwenye Taasisi ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) kwa ajili ya mafunzo na mikopo kwa vijana.

Waziri Mkuu akijibu swali hiyo amesema, serikali inatenga shilingi 15 bilioni kila mwaka kwa ajili ya kutoa mafunzo ya ujuzi na stadi za kazi kwa vijana nchini. Katika kipindi cha mwaka 2018/19 hadi 2019/20.

“Vijana 80,013 wanawezeshwa kupata mafunzo ya ujuzi wa kujiajiri na kuajiriwa hao wanapatiwa mafunzo hayo kwa njia ya uanagenzi (apprenticeship); mafunzo ya uzoefu wa kazi (internship); kutambua na kurasimisha ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi,” amejibu Waziri Mkuu.

Amesema Licha ya kuwa SIDO ni miongoni mwa taasisi za serikali zinazohusika katika utekelezaji wa mpango wa mafunzo hayo, serikali inatenga kiasi cha shilingi 1 Bilioni kila mwaka kwa ajili ya mikopo ya vijana kupitia mfuko wa maendeleo.

error: Content is protected !!