Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif ahitimisha safari ya miezi 927 duniani
Habari za SiasaTangulizi

Maalim Seif ahitimisha safari ya miezi 927 duniani

Spread the love

 

MAALIM Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, amehitimisha safari yake ya miezi 927 duniani. Anaripoti Regina Mkonde, Zanzibar … (endelea).

Mwili wa Maalim Seif, aliyezaliwa tarehe 22 Oktoba 1943 katika eneo la Nyali, lililopo Mtambwe, wilaya ya Wete, mkoani Pemba, visiwani humo, umezikwa, atika makazi yake ya milele, leo Alhamis, tarehe 18 Februari 2021.

Kuanzia alipozaliwa hadi anafikwa na mauti ni sawa na siku 28,233 ambazo ni sawa na miezi 927 na siku 16 au ni sawa na miaka 77 na miezi mitatu.

Vilio na simanzi, zilitawala eneo la Mtambwe, mara baada ya jeneza lililobeba mwili wake, lilipowasili kijijini kwako, likiwa limebebwa na askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

         Soma zaidi:-

Ilipofika, Saa 11:07 jioni, mwili wa Maalim Seif, ulingizwa kwenye nyumba yake ya milele na kuhitimisha safari yake hapa duniani, huku nyuso za majozi zikiwa zimetawala kwa

Viongozi mbalimbali wa kisiasa na kiserikali wameshiriki maziko hayo, yaliyofanyika Mtambwe, wakiongozwa na Rais wa Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi.

Wengine waliokuwepo ni Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira wa Serikali ya Tanzania, Ummy Mwalimu pamoja na viongozi wa ACT-Wazalendo, wakiongozwa na Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe.

Baada ya maziko hayo kufanyika, Serikali ya Zanzibar imesema ibada ya Hitma ya Maalim Seif, itafanyika kesho Ijumaa baada ya swala ya Alasiri, katika viwanja vya Jadija, Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Baada ya hitma hiyo kufanyika Pemba, itafanyika Unguja siku ya Jumamosi ya tarehe 20 Februari 2021, katika Uwanja wa Maisala, baada ya swala ya alasiri.

Undani wa maisha ya Maalim Seif, aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, fuatilia simulizi hii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!