May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nape aibiwa bastola Dar, yapatikana Mbeya

Spread the love

 

BASTOLA ya Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama (CCM) iliyoibwa tarehe 15 Februari 2021, katika eneo la Kawe Beach, jijini Dar es Salaam, imepatikana mkoani Mbeya. Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi tarehe 18 Februari 2021, amesema, bastola hiyo aina ya Glock 17 yenye namba YX647 ikiwa na risasi 14, ilipatikana jijini Mbeya.

Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama (CCM)

Mambosasa amesema, ushirikano kati yao na polisi wa Mbeya umefanikiwa kukamatwa kwa bastola hiyo jana Jumatano, “mtuhumiwa mmoja anashikiliwa kwa tuhuma za wizi wa silaha hiyo.”

error: Content is protected !!