Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Maajabu ya kocha mpya Simba
Tangulizi

Maajabu ya kocha mpya Simba

Spread the love

 

KLABU ya Simba inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, imefanikiwa kumpata mrithi wa Didier Gomes, ambaye ni Pablo Franco kocha kutoka nchini Hispania akiwa na uzoefu wa kufundisha klabu kubwa huku akiwa na rekodi mbalimbali. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Pablo ametambulishwa Jumamosi ya Novemba 6, 2021 kupitia kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo, ambapo kocha huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika klabu tano alizopita kama kocha mkuu, Pablo amefanikiwa kukaa katika benchi kwenye michezo 191, na katika mechi hizo amefanikiwa kuibuka na ushindi kwenye michezo 85, akipoteza michezo 64 na kwenda sare michezo 42.

Safu za ushambuliaji ambazo kocha huyo alizinoa zilifunga jumla ya mabao 300, huku safu zake za ulinzi zikiruhusu mabao 251, kutinga kwenye nyavu zake.

Klabu ya kwanza kwa Pablo kufundisha kama kocha mkuu ilikuwa ni Santa Eugenia, ambayo aliiongoza kwenye michezo 55, kushinda 21, akapoteza 24 na kupata sare 10. Kwenye klabu yake ya pili kufundisha ya Illescas, kocha huyo alihusika kwenye michezo 38, akishinda 12, na kupoteza 14 na kuambulia sare 12.

Mara baada ya hapo Pablo alijiunga na klabu ya Getafe inayoshiriki Ligi Kuu nchini Hispania, “La Liga” aliongoza kwenye michezo 14, katika mechi hizo Pablo alifanikiwa kushinda michezo miatatu, akapoteza michezo 9 na kupata sare 2.

Kwenye klabu yake ya mwisho ya Saburtalo Tribllsi ya nchini Georgia kocha huyo aliongoza timu hiyo kwenye michezo 20 na katika michezo hiyo alishinda mechi saba, kupoteza saba na kwensa sare michezo sita.

Kocha huyo amekuja kuchukua mikoba ya Gomes ambaye alivunja mkataba wake, baada ya makubaliano ya pande zote mbili kufuatia matokeo mabaya waliyoyapa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Jwaneng Galaxy.

Kibarua cha kocha huyo mpya kitaanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kati ya Simba dhidi ya Ruvu Shooting, utakaochezwa Novemba 19, 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

error: Content is protected !!