May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NBS: Mfumuko wa bei haujapanda Oktoba

Mkurugenzi Mkuu wa ofisi ya Takwimu Tanzania (NBS), Dk. Albina Chuwa

Spread the love

 

MFUMKO wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2021 umebaki kuwa asilimia 4.0 kama ilivyokuwa kwa mwezi Septemba 2021. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea)

Taarifa  hiyo imetolewa leo tarehe 8 Novemba, 2021 na Mkurugenzi wa sensa ya watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ruth Minja kuhusu fahirisi za bei za Taifa kwa mwezi Oktoba 2021.

Amesema hali hiyo inaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2021 imebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2021.

Amesema mfumko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2021 kuwa sawa na mfumko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2021 umechangiwa na kuongezeka na kupungua kwa mfumuko wa bei wa baadhi  ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Oktoba 2021 zikilinganishwa na bei za mwezi Oktoba 2020.

“Kwa mfano baadhi ya bidhaa za vyakula za vyakula zilizoonesha kupungua kwa mfumuko wa bei mwezi Oktoba, 2021 ikilinganishwa na mfumko wa bei wa mwezi Oktoba 2020 ni pamoja na maharagwe kwa asilimia 5.5, dagaa kwa asilimia 3.9, maziwa ya ng’ombe kwa asilimia 5.1 na choroko kwa asimia 2.3” ameeleza Minja.

Amesema kwa upande mwingine baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizoonesha kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa mwezi Oktoba, 2021 ikilinganishwa na bei za mwezi Oktoba ni pamoja na mavazi kwa asilimia 4.8, gesi ya kupikia asilimia 2.8, mkaa kwa asilimia 3.9 na gharama za malazi kwenye nyumba za kulala wageni kwa asilimia 5.7.

Amesema kwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba 2021 umepungua kidogo hadi asilimia 3.9 kutoka asilimia 4.0 kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2021.

“Mfumuko wa bei ambao haujumuishi bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Oktoba, 2021 umebaki kuwa asilimia 4.1 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2021” ameeleza Minja.

error: Content is protected !!