LIZ Truss anatarajiwa kuchukua nafasi ya Boris Johnson kama Waziri Mkuu wa Uingereza leo tarehe 6 Septemba, 2022 atakapokwenda kumuona Malkia Elizabeth huko Scotland. Anaripoti Felister Mwaipeta, TUDARCo … (endelea).
Truss mwenye umri wa miaka 47, baada ya kukabidhiwa mikoba, anatarajiwa kuteua mawaziri wa vyeo vya juu katika baraza lake la mawaziri ili kushughulikia mzozo wa kiuchumi na kuunganisha chama chake kilichogawanyika.
Truss alimshinda mpinzani wake Rishi Sunak katika upigaji kura wa wanachama wa uwongozi wa chama cha Conservative na kuahidi kupunguza kodi na kuwasaidia watu kulipa bili zao za nishati wakati Uingereza inakabiliwa na shida ya nishati inayoongezeka.
Truss alisema, “Nitachukua hatua madhubuti kutuvusha sote katika nyakati hizi ngumu ili kukuza uchumi wetu na kuibua uwezo wa Uingereza”.
Truss atamrithi Boris Johnson ambaye alilazimika kutangaza kujiuzulu mwezi Julai mwaka huu baada ya kashfa iliyoshuhudia uungwaji mkono kwa utawala wake kupungua na mawaziri kujiuzulu na kulazimika yeye kujiuzulu.
Leave a comment