Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu: Hatutambui kinachofanywa na NEC 
Habari za SiasaTangulizi

Lissu: Hatutambui kinachofanywa na NEC 

Tundu Lissu, Mgombea Urais Tanzania kwa tiketi ya Chadema
Spread the love

TUNDU Antiphas Mughwai Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema amesema, hakubaliani na chochote kinachoendelea kuhusu Uchaguzi Mkuu uliofanyika jana Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Lissu ametoa msimamo huo leo Alhamisi tarehe 29 Oktoba 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Tegeta jijini Dar es Salaam akiwa ameongozana na Mgombea wake mwenza, Salum Mwalimu na Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika.

Amesema, katika kampeni za uchaguzi huo zilizoanza tarehe 26 Agosti na kuhitimishwa 27 Oktoba 2020, walikutana na kadhia mbalimbali yeye pamoja na Mwalimu ikiwemo mikutano yao kuzuiwa na kupigwa mabomu ya machozi.

“Tulipigwa mabomu, kulikuwa na vizingiti kibao vya kufanya kampeni. Mgombea mwenza (Mwalimu) alipigwa mabomu mara mbili na mimi nilipigwa mabomu. Lakini, hatukukata tama tulisonga mbele,” amesema Lissu.

“Tumekwenda hivyo mpaka jana siku ya upigaji kura tuloiyoyaona na kila mmoja aliona na kusikia kilichotokea vituoni kwa mawakala wetu kuzuiwa, kuondolewa vituoni,” amesema.

Lissu amesema, suala hilo la mawakala  walilizungumza mara kadhaa hasa baada ya kuapishwa nchi nzima na kutopewa barua za utambulisho “tulijua hiki kilichotokea, kitakuja kutokea na kweli kimetoa kila mmoja ni mashahidi.”

“Katika maelfu ya vituo, mawakala wetu walikwenda katika vituo mapema tu na kuambiwa barua yako ya utambulisho haiko hapa. Kwenye vituo vingine, wakala anakuta barua ya jina lake ipo lakini picha ya mtu mwingine.”

“Maelfu ya mawakala wetu, hawakuingia kwa wakati kwenye vituo. Kuna wengine walifanikiwa kupata utambulisho lakini walipofika walizuiwa kuingia kwa kile walichoelezwa, barua ya utambulisho ilipaswa kuletwa na msimamizi wa uchaguzi,” amesema Lissu.

Akizungumza huku akirejea sheria na kanuni zinazosimamia uchaguzi huo, Lissu amesema “wengine walikaa vituoni hadi saa 9 mchana, saa 6 mchana au saa 4 asubuhi ndiyo waliruhusiwa kuingia, kabla ya kuingia, nini kilifanyika.”

“Wengine waliingia lakini ilipofika jioni wakati wa uhesabuji wa kura walitolewa nje, katika maeneo mengi jimbo la Hai polisi walipiga mabomu yaani kilichofanyika jana, hakikuwa ni uchaguzi,” amesema.

“Kilichofanyika jana, haukuwa uchaguzi, hata kwa sheria zetu zilivyo. Hili la maboksi ya kura feki si uchaguzi. Kila mahali tumeziona, Kawe hapa Dar es Salaam zimekamatwa,” amesema Lissu huku akizitoa kuzionyesha mbele ya waandishi wa habari.

John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema

“Katika uchaguzi wenye ushindani kama huu, katika uchaguzi ambao Dk. John Magufuli na wagombea wengine wa CCM walilazimika kupiga magoti kuomba kura inawezekanaje washinde kila sehemu,” amesema Lissu.

“Kilichotokea jana, siyo uchaguzi kwa kipimo chochote iwe kwa sheria za Tanzania au sheria za Kimataifa. Kama siyo uchaguzi, hatuwezi kutambua au kukubali kitu ambacho hakipo kisheria. Hatukubali na hatukubaliani kwa chochote,” amesema Lissu.

Lissu amesema “ Watanzania ambao haki yao ya kuwachagua viongozi imeibiwa, wanawajibu wa kutetea haki zao za kidemokrasia. Sisi tumefanya kile tulichoweza, tulifanya kampeni kwa nguvu zetu zote na uwezo wetu wote.”

Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara amesema “hatutakubali chochote ambacho si uchaguzi huru na wa haki.”

Ameseka, wamekwisha wasilisha malalamiko taasisi mbalimbali ikiwemo Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc), Jumuiya ya Madola na zingine za Kimataifa kuangalia kile kilichotokea kwenye uchaguzi huo.

Lissu amesema, miongoni mwa hatua zinazoweza kufanywa na taasisi hizo ni kuwekewa zuio la wale wote waliohusika na kuuhalibu uchaguzi huo kutokutoka ndani ya nchi hiyo, kufanya miamalaka ya kimataifa au biashara.

1 Comment

  • Vituo vimefungwa saa 10jioni, uhesabuji kura kituoni unafanyika na pengine kumalizika saa 2 hadi 5usiku, msimamizi wa uchaguzi wa kituo anayapeleka katani kisha jimboni. Katika mazingira na mwenendo huu inawezekanaje matokeo ya kura ya mbunge yawe tayari saa 8 za usiku na mshindi kutangazwa masaa machache tu baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa? Hapana. Hii ni wazi kabisa, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo husika alikuwa na matokeo yake. Hii ndiyo imetikea jimbo la Arusha, Hai, Kawe, Mbeya na kwingine..!!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!