Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa  Lissu amtetea Dk. Mashinji 
Habari za Siasa

 Lissu amtetea Dk. Mashinji 

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vicent Mashinji
Spread the love

MWANASHERIA Mkuu wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema) ameikosoa serikali kuhusu namna inavyoshughulikia suala la uchochezi   katika serikali ya awamu ya tano, anaandika Victoria Chance.

Akiongea na waandishi wa habari  katika Makao Makuu ya Chadema Kinondoni Jijini Dar Es Salaam Lissu ameorodhesha  matukio mbalimbali ambayo serikali inadai kuwa ni ya uchochezi, orodha ambayo Lissu anaipinga.

Alianza kwa kuelezea  kwamba kuna utaratibu unaondaliwa ili kumfikisha Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa mahakamani kwa kosa la uchochezi kama ambavyo  mwalimu Julius Kambarage Nyerere alishtakiwa enzi za ukoloni wakati hakuwa na hatia.

Aidha Lissu alieleza kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vicent Mashinji, aliwekwa ndani kwa sababu hiyo hiyo ya uchochezi. Tayari Dk. Mashinji amepewa dhamana ya polisi huko Mbamba Bay, mooani Ruvuma, alikokuwa amekamatiwa na polisi.

Lissu ameongezea kuwa, “Wabunge wetu kadhaa akiwemo Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, na Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea,  amabao either (ama) wamekamatwa au kushtakiwa kwa makosa yanayofanana na hayo.”

Aliendelea, “Na kuna wanacahama zaidi ya 51 wa Wilaya ya Chato wamekatwa kwa sababu ya kufanya kikao cha ndani wakati dikteta uchwara akiwa likizo.”

Pia aliendelea  kuelezea kuwa kuna mamia ya watu wamewekwa ndani kwa kosa la kutumia simu zao kutuma ujumbe wa maandishi ambao haumpendezi Rais Magufuli na wapambe zake.

Kadhalika, alisema kuwa mnamo tarehe 29 Juni mwaka jana yeye mwenyewe alishtakiwa kwa kosa hilo hilo la uchochezi.

Kutokana na hayo Lissu amemalizia kwa kusema kwamba, “Rais Magufuli anatakiwa kupingwa  na ajue kwamba nchi hii inakatiba,  na kwamba, wale watakao muunga mkono katika haya ni dhahiri watakuwa hawana akili.”

Lissue amawahimiza Watanzania kipaza sauti zao kwani mahali tulipofikishwa sio salama kisiasa.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!