Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kwa heri Pascal Ndejembi, utakumbukwa kwa mengi
Habari za SiasaTangulizi

Kwa heri Pascal Ndejembi, utakumbukwa kwa mengi

Pancras Ndejembi
Spread the love

WINGU zito limetanda katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, kutokana na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa  Chama hicho Mkoani hapa na Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Chama hicho mkoani Dodoma, Pancras Ndejembi (84) kufariki Dunia. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Ndejembi alifariki jana Jijini hapa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alipokuwa amelazwa baada ya kupelekwa hospitalini hapo juzi kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana Jijini hapa, Mweyekiti wa Chama hicho Mkoani hapa, Godwin Mkanwa, alisema wamepokea kwa masikitiko kifo cha mwanasiasa huyo kwani alikuwa ni mhimili wa ushauri kwa viongiozi wa kisiasa.

“Natoa pole kwa familia, sisi chama mkoa tumepokea kwa masikitik na mshtuko mkubwa kifo chake ukizingatia alikuwa na afya njema na baada ya afya yake kubadilika na kupelekwa hospitali, madaktari wamehangaika ila kunusuru uhai wake lakini imeshindikana na ametangulia mbelea ya haki.

“Yeye kama mshauri wetu mkuu katika mkoa na mmoja wa wazee katika baraza la wazee tutakosa mchango wake wa kisiasa na busara zake,” alisema Mkanwa.

Akimzungumzia zaidi Marehemu, Mwenyekiti huyo, alisema wakati wa uhai wake alikuwa muumini wa kweli wa chama, alikuwa mwadilifu, muaminifu na muelekezaji pindi mambo yanapoenda kombo.

Alisema Marehemu Ndejembi ndiye ambaye ameifanya Dodoma kuwa ngome ya Chama cha Mapinduzi.

“Ameifanya CCM kuwa ngome imara mara kadhaa alikuwa akiasa tusiyumbishwe hasa ujio wa vyama vingi, vilipoanza yeye alikuwa kinara kwa kuhimiza tushikamane kwa pamoja kukijenga chama chetu  na kwa uhakika yeye ametoa mchango mkubwa sana kiasi kwamba ngome ile sasa imezidi kuwa imara mpkaka leo,” alisema.

Alisema katika mambo ya siasa anayokumbuka kwa Marehemu ni kuwaunganisha viongozi wa kisiasa pamoja na kuujengea heshima Mkoa wa Dodoma.

“Ninachokikumbuka ni kule kutuunganisha mkoa kuwa wa moja hasa sisi viongozi, lakini pia kuijengea heshima kama Dodoma na mara kadhaa amekuwa mstari wa mbele amehakikisha Dodoma inabaki kwenye kumbukubmu,” alisema.

Mwenyekiti huyo aliwaomba wana CCM kuwa wamoja katika kipindi hichi kigumu pamoja na kuyaenzi yale mazuri yaliyofanywa na marehemu.

“Niwaombe wana-CCM tuzidi kumuenzi kwa mema aliyokuwa nayo na juhudi alizozozionyesha waziwazi tuziendeleze na juhudi zake za kukijenga chama hapa mkoa na kufanya kuwa ngome basi tumuenzi kwa hilo,”alisema.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mtoto wa Marehemu, Augustino Ndejembi alisema baba yao amefia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa mtoto huyo alisema awali alilazwa katika Hospitali ya DCMC Ntyuka Jijini hapa na kuruhusiwa Desemba 26 mwaka huu.

Alisema walimrudisha nyumbani lakini juzi hali yake ilibadilika na kumpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma ambapo jana asubuhi hali yake ilizidi kuwa mbaya na kisha mauti kumkuta.

Augustino alisema Marehemu atazikwa kijijini kwake katika eneo la Bihawana nje kidogo ya Jijini la Dodoma pembeni ya kaburi la baba yake.

“Bado tuna ndugu wengi hawajafika Dodoma kwahiyo siku ya kuzika bado haijajulikana ila atazikwa katika eneo la Bihawana jirani na kaburi la baba yake,”alisema.

Historia

Marehemu Ndejembi alizaliwa mwaka 1934 Bihawana Dodoma, ambapo amewahi kuwa Mwalimu katika Middle School katika shule za Bihawana na Kibakwe.

Pia amewahi kufanya kazi katika Serikali ya awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kisha kuwa Mkuu wa Wilaya katika Wilaya za Tanga, Rombo na Moshi Mjini.

Marehemu Ndejembi alikuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma kuanzia mwaka 1982 mpaka 2007 ambapo alimwachia William Kusila na kisha Adam Kimbisa na sasa ni Godwin Mkanwa.

Pia amewahi kuwa Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM kwa miaka kadhaa katika utawala wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu, Benjamini Mkapa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!