Tuesday , 30 May 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri Mkuu aagiza wakazi wa Dodoma kulipwa fidia
Habari za Siasa

Waziri Mkuu aagiza wakazi wa Dodoma kulipwa fidia

Spread the love

WAZIRI Mkuu Kasimu Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi kuweka utaratibu wa kuwafidia watu wanaopisha maeneo yao. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Majaliwa ametoa maagizo hayo jana alipokuwa akizungumza na wananchi na wafanyabiashara wa eneo la Mjimpya waliopisha ujenzi wa bustani.

Waziri Mkuu alifanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ambayo yametengwa kama sehemu ya maegesho ya magari makubwa ya mizigo pamoja na sehemu ya bustani ya kupumzikia.

Katika ziara hiyo Majaliwa alisema kuwa kutokana na kuwa Dodoma kuwa makao makuu ni lazima mji ukapangwa vizuri na kuwa na vivutio vya kutosha kulingana na adhi ya makao makuu yannchi.

“Hatuwezi kuacha Dodoma iwe kama Dodoma ya zamani ni lazima iboreshwe na kwa maana hiyo ni lazima iwe na vivutio. Pamoja na hayo mkurugenzi nakuagiza kuangalia uwezekano mzuri wa kuwa patia maeneo watu ambao wamepisha maeneo yao.

“Na kama hilo halitoshi mkurugenzi weka utaratibu mzuri wa wafanyabiashara waliopisha sehemu zao kuwapangia maeneo vizuri ya kufanya biashara kama ilivyokuwa awali,” alisema Majaliwa.

Katika hatua nyingine Majaliwa amewataka wakazi wa Jiji la Dodoma kuwa waaminifu katika kutunza mazingira sambamba na kutumia fursa ya Dodoma kuwa makao makuu kwa ajili ya kufanya kazi na kujiongezea kipato.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji Godwin Kunambi,amesema kuwa kwa sasa kuna kiasi cha sh.Bilioni 77.5 kwa ajili ya kujenga maeneo ya viburudisho.

Alisema kwa sasa inajengwa sehemu ya kivutio sehemu ya Chinangali ambapo zitapatikana burudani zote ikiwa ni pamoja na sehemu ya mikutano ya viobgozi.

Mbali na hilo alisema kuwa kwa sasa Jiji la Dodoma litakuwa kati ya Majiji ya mfano ambalo litawafanya watu mbalimbali kutoka maeneo kufika kupumzika.

“Serikali imeamua kulifanya Jiji la Dodoma kuwa Jiji la mfano na itakuwa sehemu ya kufika na kupumzika na kama mtu alikuwa na shida na matatizo yake akifika atasahau matatizo yake,” alisema Kunambi.

Kuhusu vijana Kunambi aliwataka vijana kujitokeza kwa ajili ya kujiunga vikundi na kuomba mikopo kwani ofisi yake ina zaidi ya bilioni moja kwa ajili ya mikopo ya vijana,akina mama na watu wenye ulemavu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Uamuzi juu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi 13 Juni

Spread the love  MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR), imepanga...

Habari za Siasa

Musoma Vijijini waomba ujenzi wa barabara uanze haraka

Spread the loveJIMBO la Musoma Vijijini, mkoani Mara, limeomba Serikali kuhakikisha ujenzi...

Habari za Siasa

ACT Wazalendo yaanika madudu miradi ya ujenzi, moundombinu

Spread the loveCHAMA cha ACT Wazalendo kimeeleza wasiwasi juu ya uelekeo wa...

Habari za Siasa

Samia ashuhudia utiaji saini ujenzi wa minara 758 ya bilioni 265

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa kampuni za...

error: Content is protected !!