Saturday , 10 June 2023
Home Kitengo Michezo Kocha Mkuu Simba: Kundi letu lipo wazi
Michezo

Kocha Mkuu Simba: Kundi letu lipo wazi

Patrick Aussems, Kocha Mkuu wa Simba
Spread the love

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amsema kuwa bado timu yake inanafasi ya kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika kutokana na kundi hilo kuonekana lipo wazi kwa timu yoyote kuweza kusonga mbele. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Kocha huyo amesema hayo kupitia kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter mara baada tu Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika CAF kupanga makundi hayo ya ligi ya mabingwa na Simba kuangukia kwenye kundi D, sambamba na klabu za Al Ahaly (Misri), As Vital (Congo DRC) na JS Saoura (Algeria).

“Kundi hili lipo wazi :Michezo ya kusisimua!! … Na kiukweli tunanafasi nzuri ya kufika robo fainali, kwa hiyo tunahitaji kuwa pamoja.”

Makundi hayo yalipangwa jana kwenye mji wa Cairo, Misri yalipo makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ambapo Simba iliwakilishwa na mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo, Salim Abdallah ambapo mchezo wao wa awali wataanzia nyumbani Dhidi ya JS Saoura ya nchini Algeria.

Simba imefuzu kwenye hatua hii mara baada ya kuwatoa klabu ya Nkana FC kutoka nchini Zambia kwa jumla ya mabao 4-3 katika michezo yote miwili waliocheza nyumbani na ugenini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

MichezoTangulizi

Benki ya NBC yakabidhi kombe la ubingwa wa ligi kuu kwa Yanga

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa ligi ya NBC, Benki ya Taifa ya...

HabariMichezo

Benki ya NBC yazindua kombe jipya la Ligi Kuu Tanzania Bara

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa Ligi ya NBC , Benki ya Taifa...

MichezoTangulizi

Yanga malizeni ugomvi na Fei Toto – Rais Samia

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia...

Michezo

Samia aipongeza klabu ya Yanga kwa hatua iliyofikia

Spread the love RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia...

error: Content is protected !!