Tuesday , 3 October 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kuelekea Uchaguzi Serikali za Mitaa, wanawake waaswa
Habari za Siasa

Kuelekea Uchaguzi Serikali za Mitaa, wanawake waaswa

Spread the love

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Kibena Kingo amewataka Madiwani wanawake nchini kuzidisha upendo baina yao na kuacha unafiki jambo litakalowasaidia kushika nafasi za uongozi kwenye kata zao na kukamilisha dhana ya Serikali ya 50 kwa 50. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Kingo ambaye pia ni Diwani wa kata ya Ngerengere wilayani humo, alisema hayo jana wakati akizungumza na baadhi ya madiwani wanawake na wa viti maalum walioshiriki warsha ya siku tatu kwa wanawake watia nia ya kugombea uwenyeviti wa vijiji na vitongoji katika uchaguzi wa Serikali za mitaa iliyoandaliwa na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP- Mtandao).

Diwani huyo alisema, akiwa diwani kamili anaamini suala la upendo na kutokuwa na unafiki linaweza kumfanya kiongozi kuzidi kukua katika nyadhifa mbalimbali za uongozi.

“Jifunze kukaa kimya na sio kila jambo unalosikia au kuliona unatakiwa uliseme, unatakiwa uangalie la kuongea na mahali la kuongea,” alisema Kingo.

Aidha alisema, wilaya ya Morogoro ina jumla ya kata 31 za uchaguzi na kwamba mpaka sasa wanawake wameshika kata 6 ambapo anatarajia katika uchaguzi ujao mwakani wanawake wataendelea kushika nafasi na kufikia hata kata 10 zenye madiwani wanawake.

Hata hivyo aliwataka wanawake kutambua kuwa 50 kwa 50 haiji kwa kusubiriwa bali kwa kuidai na kuitafuta ambapo aliwataka kutokubali kubaguliwa ili kufikia lengo linalokusudiwa.

Aliwaasa madiwani ambao ni walezi wa kata kuendelea kuwa walezi wazuri kwa kata zao na watu wake kwani kufanya hivyo kutawaongezea imani wapiga kura.

“Mlio walezi wa wagombea wa nafasi za chini mnapaswa kutambua, wagombea viijini mwetu uwezo wao ni mdogo sana, wanapaswa kusaidiwa kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwemo za kibinadamu wanazokumbana nazo kabla ya kuchaguliwa, ikiwemo ugomvi wa wanawake kisimani ambao wengine wamekuwa wakiubebea mwao na kumbe wanapaswa kuuacha,” alisema Kingo.

Pia Kingo, aliwakumbusha  wanawake kujenga dhana ya kuacha na kuvunja  makundi baada ya uchaguzi na kurudi kuwa wamoja katika kata, kitongoji au kijiji jambo ambalo humsaidia kiongozi yeyote yule kupiga hatua zaidi.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Rehema Saidi Bwasi aliwataka washiriki hao kwenda kuyatumia vyema mafunzo hayo waliyopewa ili kupata kushika nafasi mbalimbali za uongozi ambazo haziji bila ushirikiano kwa lengo la kupata usawa wa 50 kwa 50.

Awali mwezeshaji wa warsha hiyo kutoka TGNP, Dk. Consolata Sulley alisema, lengo la warsha hiyo ni kuwajengea uwezo wanawake wa Wilaya hiyo waliotia nia katika kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Dk. Sulley ambaye pia ni Mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam alisema warsha hiyo pia imelenga kuwatoa hofu na kuwatia moyo sambamba na kuwafahamisha namna mchakato wa uchaguzi unavyotaka mtu kuwa na moyo wa ujasili tofauti na hali ilivyo mara nyingi mwanamke amekuwa akionekana kuwa muoga.    

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bilioni 6.1 kumaliza tatizo la maji Katoro-Buseresere – Geita

Spread the loveMakamu mwenyekiti wa Umoja wa wanawake CCM, (UWT), Zainab Shomari...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kupokea ndege ya 14 ya ATCL, safari kuongezeka

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania, kesho tarehe 3 Oktoba 2023, inatarajia...

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

error: Content is protected !!