April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Maleria yaahirisha kesi ya wafugaji, askari

Spread the love

MAHAKAMA ya Mwanzo Mikongezi, Mvomero imelazimika kuahirisha kesi ya kujeruhi iliyowahusisha wafugaji watatu waliowajeruhi askari wanyamapori sehemu mbalimbali za miili yao baada ya mashahidi wanne upande wa washtakiwa kutofika mahakamani wakidaiwa kuumwa ugonjwa wa Malaria. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Hakimu wa Mahakama hiyo, Mussa Lilingani alisema, amelazimika kuahirisha kesi kutokana na mashahidi hao kutofika mahakamani ambapo aliagiza itolewe hati ya kukamatwa kwa washtakiwa wengine watatu ambao walikimbia baada ya tukio hilo.

Awali Hakimu huyo aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Sperwa Kisakiri, Daniel Babalai na Kashuma Kishaki ambapo alisema, siku ya tukio washtakiwa hao waliwajeruhi Emmanuel Willnely na Exavery Pius ambao ni askari wa kamati ya wanyamapori ya maliasili ya kijiji, kwenye msitu wa hifadhi wa asili wa kijiji cha Kihondo kata Doma wilayani humo walipokuwa wakiondoa mifugo iliyoingia hifadhini kinyume cha sheria.

Tukio hilo lilitokea Oktoba 8 mwaka huu katika msitu huo wa hifadhi ambapo Kesi ya kujeruhi namba 115/2019 yenye kifungu namba 228 ilisomwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Oktoba 11, ambapo itasikilizwa tena Oktoba 30 mwaka huu.

error: Content is protected !!