Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kongamano la kina Dk. Slaa kupinga mkataba bandari lakwaa kisiki
Habari za SiasaTangulizi

Kongamano la kina Dk. Slaa kupinga mkataba bandari lakwaa kisiki

Balozi, Dk. Willbroad Slaa
Spread the love

KONGAMANO la kujadili mkataba wa bandari na upatikanaji katiba mpya, lililoandaliwa na wanaharakati akiwemo Dk. Wilbroad Slaa, kwa kushirikiana na taasisi ya Tanzania Transparent Forum, limekwaa kisikii baada ya kukosa ukumbi wa kuufanyia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online kwa simu, leo tarehe 4 Oktoba 2023, Dk. Wilbroad Slaa, amesema kongamano hilo limekwama baada ya kila ukumbi wanaokodisha kwa ajili ya kulifanya, wamiliki kukataa dakika za mwisho ,kisha kuwarejeshea fedha zao.

“Ndiyo kongamano letu limeahirishwa kwa namna ya ajabu sana, mbinu waliyokuja nayo ni ya kuwaingia wale watu wenye ukumbi, dakika za mwisho watu wa ukumbi wanaturudishia hela. Hadi jana usiku kumbi mbili ziliturudishia fedha zetu bila kutoa sababu za msingi,” amedai Dk. Slaa.

Alipoulizwa sababu za kongamano hilo kukwamishwa, Dk. Slaa alijibu “tunajua kwamba Serikali haitaki kitu chochote chenye sura ya demokrasia, wala haitaki kumung’unya maneno katika hili. Hawataki tuzungumzie habari ya bandari na ya katiba.”

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alisema vikwazo hivyo havitawarudisha nyuma kwani wana mbinu nyingine zaidi ya 1,000 kufikisha ujumbe wao kwa watanzania kuhusu masuala hayo.

“Tutatumia mbinu zetu zote mpaka zifike 1,000 na nina hakika hapo katikati zitafanikiwa. Mbinu hizo ni siri siwezi kuzitoa hadharani, lakini tutazitumia ilimradi tunalinda bandari zetu, hakuna mtu hata mmoja atagusa, hatutakabidhi bandari kwa mtu yeyote yule na masuala ya katiba tutayazungumza,” amesema Dk. Slaa.

Dk. Slaa na wenzake wamekuwa wakipaza sauti katika namna mbalimbali kupinga mkataba wa uwekezaji bandarini unaotarajiwa kufanywa na kampuni ya Imarati ya Dubai, Dubai Port World(DP World), wakiitaka Serikali iuvunje kwa madai kuwa hauna maslahi kwa taifa.

Hata hivyo, katika nyakati tofauti Serikali imetoka hadharani na kuwaeleza wananchi kwamba mkataba huo una maslahi kwa taifa na kwamba dosari zilizoibuliwa na wadau mbalimbali itazirekebisha ili kuuboresha zaidi.

Kwa upande wa katiba mpya, Slaa na wenzake wanaitaka Serikali ianze mara moja kukufua mchakato wa upatikanaji wake, kwa kuanzia pale ambapo uliishia mnamo 2014.

Wanapinga mpango wa Serikali kuanza kutoa elimu ya katiba katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo (2023-2026), wakidai uamuzi huo unalenga kukwamisha mchakato huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

Habari za Siasa

Serikali yawapa maagizo Ma-RC udhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Spread the loveWAKUU wa mikoa nchini wametakiwa kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wananchi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

error: Content is protected !!