Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kituo cha watoto yatima chafanya dua maalum kwa Samia
Habari Mchanganyiko

Kituo cha watoto yatima chafanya dua maalum kwa Samia

Spread the love

KITUO cha  kulelea watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu cha Mwana Orphan Islamic kilichopo Kata ya Vigunguti Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam kimefanya dua maalumu ya kuwaombea viongozi wa Serikali na Dini kuendelea kuwa na amani na utulivu. Anaripoti Faki Ubwa… (endelea).

Akizungumza wakati wa dua hiyo iliyofanyika kituoni hapo wiki iliyopita, Shekhe Ahmed Kandauma, Mwenyekiti wa Vijana kwenye Baraza la Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA, amesema kwamba dua hiyo imelenga kudumisha amani na kulifanya Taifa liwe salama,hususani katika kipindi hiki cha zoezi la sensa na makazi linalotarajiwa kufanyika agost 23 Mwaka huu.

Sheikh Kanduma alisema kwamba sensa ilianza kwa mtume Muhamad, “katika hadithi sahihi za Mtume Muhammad (S.A.W) amesema mtume alihitaji idadi ya maswahaba zake ,aliwaita na kuwahesabu kwa makundi ,hivyo inaonesha mfano wa sensa kwamba imeanza tangu enzi za Mtume Muhammad (S.A.W)” .

Amesema kuwa yatima hao wamefanya dua kwa viongozi  ambayo italipa nuru zaidi taifa .

“Kitendo kilichofanywa na kituo hicho kufanya dua kwa viongozi wa serikali na dini ikiwemo Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wake Dk. Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ,Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibari Dk Hussein Mwinyi pamoja na Taifa kwa ujumla ni jambo la kuigwa na kutiliwa mfano Kama ambavyo kituo hicho kimeandaa dua hiyo”

Kwa upande wake Mwanzilishi wa Kituo hicho kilichoanzishwa Mwaka 2005, Saada Ally Omary amesema kwamba kituo hicho kinaidadi ya Watoto 50 kwasasa Kati yao Watoto wakike ni 23  huku wa kiume wakiwa 27, nakwamba Watoto 21 wanasoma shule za bweni,na Watoto 13 wanasidiwa na kituo hicho wakiwa wanaishi kwa bibi zao.

Saada amesema kuwa kituo hicho kimefanikiwa kuzalisha Watoto waliofika elimu ya juu kwa maana ya astashahada,stashahada,na shahada, kupata kiwanja kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani kwa ajili ya kujenga kituo kitakachojitosheleza kwa maana ya kuwa na shule,mabweni ,zahanati,na viwanja vya kuchezea kwa Watoto yatima,Kuiunganisha jamii ya wakazi wa Vingunguti na sehemu za karibu kwa vile wanavyojitoa na kukiangalia kituo hicho.

Aidha ameongeza kuwa kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo  kukosekana kwa fedha ya kulipa kodi ya pango ya jengo linalotumika kwasasa.

Pia kina ukosefu wa fedha za kujenga kituo chao huko Mkuranga Mkoani Pwani, uhitaji wa vifaa vya masomo kama mabegi, madaftari na sare za shule, uulipaji wa bili za umeme na maji,Uhitaji wa vyakula na mavazi, uhitaji was huduma ya afya na bima, uondoaji wa maji taka kila baada ya mwezi.

“Naiomba jamii pamoja na wahisani mbalimbali kuweza kujitokeza kukisaidia kituo chetu kwani bado kunauhitaji mkubwa wa huduma kwa Watoto wanaolelewa katika kituo hiki,pamoja na kutuwezesha  kufanyika kwa ujenzi wa kituo kitakachojitosheleza katika kiwanja cha Mkuranga Mkoani Pwani  ili kuondoa adha wanazozipata Watoto hao” alisema Saada.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!