Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari Shirika la Camillians lapata Mafratel wapya, waweka nadhiri ya kwanza
HabariHabari Mchanganyiko

Shirika la Camillians lapata Mafratel wapya, waweka nadhiri ya kwanza

Spread the love

VIJANA watatu wa Kitanzania, wamefanikiwa kujiunga na Shirika la Kanisa Katoliki la Wahudumu wa Wagonjwa (Camillians) Tanzania na kuweka nadhiri zao za  kwanza. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mafrateli hao ni Vitus Paul Ndwangira, Joseph Gervas Modest na Adam Edward Luhamo ambao waliweka nadhiri zao za kwanza juzi katika Kanisa Katoliki la Shirika hilo la Camillians, lililopo Parokia ya Mt. Yohana wa Mungu, Yombo Vituka, jijini Dar es Salaam.

Mafratel hao, waliweka nadhiri zao juzi tarehe 21 Agosti, 2022 mbele ya Mkuu wa Shirika hilo nchini, Padre Festo Atanas Liheta  na kushuhudiwa na umati wa ndugu, jamaa na marafiki wa mafratel hao ambao wengi walitoka mikoani kushuhudia tukio hilo la kihistoria kwao.

Misa ya Takatifu ya kuwapokea vijana hao, iliongozwa na Padre Liheta Mkuu wa Shirika, huku mahubiri yakitolewa na Padre Joseph Mashauri ambaye pia ni Paroko wa Kanisa la Mt.  Rita, Goba jijini Dar es Salaam.

Mapadre wengine waliohudhuria sherehe hizo ni Padre Shukrani Mbilingenda M.I, Padre Patrick Atanas Bwakila M.I Paroko Msaidizi Parokia ya Bikira Maria Salama ya Wagonjwa Muhimbili, Padre Godfrey Pandula M.I Paroko Msaidizi Parokia ya Mt Karoli Lwanga Dovya, Padre Mushi Safari M.I Paroko wa Parokia ya Yohane wa Mungu Yombo Vituka na Padre Innocent Gwalasa M.I Paroko Msaidizi Parokia ya Mt. Yohane wa Mungu Yombo Vituka.

Wengine ni Padre Gasper Lifa Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Fransic wa Assiz, Ebuyu jimbo la Mahenge na Paroko wa Parokia ya Bunduki wa Jimbo la Morogoro.

Misa hiyo ilifuatiwa na halfa ya kukata na shoka iliyofanyika katika viwanja vya Kanisa hilo ambapo kulikuwa na burudani mbalimbali za kuwapongeza mafratel hao.

Kwa hatua hiyo waliyofikia vijana hao,  wamejitoa kuishi maisha ya kiinjili kwa nadhiri ya usafi wa moyo, utii, umaskini na kujitolea maisha yao kwa kuhudumia wagonjwa hata katika hatari ya  maisha yao wenyewe.

Vijana hao sasa wataenda kujiunga na Chuo Kikuu cha Jordan kwa masomo ya theology kwa muda wa miaka minne

Kwa sasa, shirika la Camillians wanafanya huduma katika Parokia ya Mt. Nikolaus Mikese jimbo la Morogoro, Parokia ya Muhimbili Parokia ya Bikira Maria Salama ya Wagonjwa, Parokia ya Mt. Kamili Yombo Kiwalani, Parokia ya Yohane wa Mungu Yombo Vituka, Parokia ya Mt. Rita wa Akashia Goba na Parokia ya Karoli Lwanga Yombo Dovya.

Parokia hizo zipo chini ya Mapadre wa shirika la Mtakatifu Kamili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!