Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kinana: Kiswahili ni lugha ya ukombozi Afrika
Habari Mchanganyiko

Kinana: Kiswahili ni lugha ya ukombozi Afrika

Spread the love

 

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amesema kuna Ushahidi wa kila aina kuwa Kiswahili ndiyo lugha ya ukombozi Afrika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kinana ameyasema hayo leo Jumatano tarehe 6 Julai, 2022, wakati akiwasilisha mada katika kongamano kuelekea siku ya Kiswahili duniani lililofanyika jijini Arusha.

Mkongwe huyo wa siasa nchini amesema moja ya chombo kilichosaidia ukombozi wa Tanzania ni Kiswahili na kikatumika pia kwa ukombozi wa nchi za kusini mwa afrika na Afrika Mashariki.

Amesema ni Kiswahili ndicho kilichowezesha kupatikana kwa uhuru wa Tanzania mapema “ni mchango wa lugha ya Kiswahili katika shughuli nzima ya ukombozi kwasababu wote tulikuwa tunazungumza kiswahili viongozi na wananchi wanawasiliana.”

Amesema ni Kiswahili kilitumika katika mikutano ya hadhara, ujumbe kupitia redio ulifikishwa kwa Kiswahili “kwaiyo tulikuwa na lugha iliyotuwezesha kuwasiliana kwa urahisi sana.”

“Hivyo kuna haja ya kukumbuka na kukubali kwamba lugha ya Kiswahili hapa Tanzania imetoa mchango mkubwa sana katika kuharakisha ukombozi wa Taifa letu.”

“Wote ni mashahidi kwamba Baba wa Taifa na viongozi wa TANU wakati ule walizunguka nchi nzima kuzungumza na wananchi juu ya harakati za ukombozi, harakati za kutafuta uhuru na jambo hili lilitusaidia sana waliwaelewa viongozi haraka na kuwasilina kwa umakini na tukapata uhuru wetu haraka sana,” amesema Kinana.

Amesema hata baada ya uhuru Kiswahili kilisaidia kujenga umoja wa kitaifa, umoja wa nchi yetu tulionao moja ya sababu kubwa ni lugha ya Kiswahili kwamba sote tunawasiliana kwa lugha ya Kiswahili.”

“Lugha hii vilevbile imesaidia sana ukombozi wa Kusini mwa Afrika ziko baadhi ya nchi ambao raia wao wanazungumza Kiswahili na ambao sehemu ndogo sana ya wananchi wanazungumza Kiswahili,”

Ametolea mfano Msumbiji raia wengi hawazungumzi Kiswahili lakini raia wengi wanaoishi kaskazini mwa nchi wanazungumza Kiswahili na ndiko kulikoanzia harakati za ukombozi katika jimbo la Kadolgado jimbo ambalo linapakana na Tanzania.

Amesema ilikuwa rahisi kutumia Kiswahili kuanzisha ukombozi wa baadhi ya nchi kusini mwa Afrika. “Nchi hizi ambazo zilikombolewa chombo kikuu ambacho kilisaidia ni majeshi yao,” Amesema majeshi hayo yalifanya mafunzo kwa Kiswahili.

“Kwasababu walitoka nchi zinazozungumza lugha tofauti wanajeshi waliamua kutumia lugha ya Kiswahili kama njia ya mawasiliano na kufundishia masuala ya jeshi, kufundishia mikakati, matumizi ya silaha.

“Ikawa ndiyo lugha ya kimapigano lugha ya majeshi ya ukombozi kusini mwa Afrika, ni dhahiri kwamba mkiwa na umoja na kwenye jeshi maelewano ni jambo muhimu sana la sivyo mtauana wenyewe. Kwahiyo nafasi ya Kiswahili imekuwa kubwa katika ukombozi kusini mwa Afrika,” amesema Kinana.

1 Comment

  • Hongera kwa hili!
    Profesa George Mhina aliwahi kusema, “Taifa lisilo na lugha yake, ni taifa mfu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!