August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maandalizi Sensa yafikia asilimia 87 zikiwa zimebaki siku 48

Kamishna wa Sensa na Makazi ya Watu Tanzania, Anna Makinda

Spread the love

 

MAANDALIZI Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti mwaka huu, yamefikia asilimia 87 ikiwa zimebaki siku 48 kufika siku ya Sensa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma …(endelea).

Aidha tathimini iliyofanyika imebaini wananchi asilimia 97 wapo tayari kuhesabiwa katika sensa ya watu na akazi tofauti na ile ya mwaka 2012 ambapo tathimini ilionesha watu asilimia 80 ndio waliokuwa tayari kuhesabiwa.

Hayo yamebainishwa leo Jumatano tarehe 6 Julai, 2022, na Mtakwimu mkuu wa Serikali, Dk Albina Chuwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kwa mafunzo ya wakufunzi wa Sensa ya Watu na Makazi.

Dk.Chuwa amesema kuwa mafunzo kwa ngazi ya taifa yamekamilika ambapo yalifanyika kwa siku 21 kuanzia tarehe 10 hadi 30 Juni mwaka huu.

Amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo na uelewa wa pamoja washiriki wote kuhusu nyenzo zote za sensa pamoja na utaratibu mzima wa kufanya sensa ya watu na makazi, sensa ya majengo na sensa ya anuani za makazi ili waweze kwenda kufundisha katika ngazi za Mkoa.

Amesema kuwa washiriki wa mafunzo katika ngazi ya taifa walikuwa ni wataalam kutoka katika Wizara,Idara na taasisi za serikali,wawakilishi kutoka vyama vya watu kwenye ulemavu na wawakilishi kutoka sekta binafsi na vyuo vikuu.

Aidha amesema hatua inayofuata ni mafunzo katika ngazi ya mkoa ambayo yameanza rasmi leo katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.

“Mafunzo haya yatafanyika kwa siku 21 kuanzia tarehe 06 hadi 26 Julai, 2022, washiriki wakiwa ni wataalam kutoka TAMISEMI ikiwa ni pamoja waratibu wa sensa wa wilaya, maafisa elimu mkoa na wilaya, wataalamu wa TEHAMA wa wilaya, Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya, Maafisa Mipango wa Wilaya, Waratibu Elimu Kata, pamoja na wawakilishi kutoka vyama vya watu kwenye ulemavu nchini,” ameeleza Dk.Chuwa.

Katika maelezo yake Dk Chuwa amesema kuwa baada ya mafunzo hayo washiriki watakaofaulu watakuwa na wajibu wa kwenda kufundisha wasimamizi wa makarani wa sensa ngazi ya wilaya ,tarafa, shehia kwa muda wa siku 21 kuanzia tarehe 29 Julai hadi tarehe 18 Agosti 2022.

error: Content is protected !!