Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kina Mbowe wasomewa mashtaka upya, DPP hajakamilisha taratibu
Habari za SiasaTangulizi

Kina Mbowe wasomewa mashtaka upya, DPP hajakamilisha taratibu

Freeman Mbowe akiwa mahakamani
Spread the love

 

KIONGOZI wa chama kikuu cha upinzania nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, wamesomewa upya mashtaka katika kesi ya ugaidi inayowakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mbowe na wenzake wamesomewa mashtaka hayo upya leo Ijumaa tarehe 6 Agosti 2021, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba na afisa kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtka nchini humo (DPP), Pius Hilla.

Hakimu Simba, ametoa uamuzi huo kwa kuwa washtakiwa hao walisomea mashtaka wakiwa tofauti. Mbowe ambaye ni mshhtakiwa wa nne ameunganishwa katika kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka 2020.

Hata hivyo, washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlama ya kusikiliza mashtaka ya ugaidi na uhujumu uchumi yanayowakabili.

Mbali na mbowe, washtakiwa wengine; ni Halfani Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa na Mohammed Abdillahi Lingwenya.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 13 Agosti 2021 baada ya upande wa Jamhuri kudai ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hijakamilisha taratibu za kuifungua kesi hiyo kwenye mahakama yenye mamlaka ya kusikiliza ambayo ni Mahakama Kuu.

Mbowe na wenzake, wamesomewa mashitaka matano, shtala la kwanza ni kula njama za kufanya ugaidi linawakabili wote wanne, ambapo wanadaiwa kwenda kinyume na sheria ya kuzuia ugaidi na uhujumu uchumi.

Wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya tarehe 1 Mei na 1 Agosti 2020 katika maeneo mbalimbali, ikiwemo Hotel ya Aishi mkoani Kilimanjaro. Mkoani Dar es Salaam, Morogoro na Arusha.

Kosa la pili linamkabili Mbowe pekee, anadaiwa kufadhili vitendo vya ugaidi kwa kutoa fedha za kufadhili ugaidi. Mbowe anadaiwa kutenda kosa hilo 1 Agosti 1 2020 akiwa katika hoteli ya Aishi.

Shtaka la tatu, linamkabili Adam la kumiliki silaha kinyume cha sheria anadaiwa kutenda kosa hilo tarehe 5 Agosti mwaka 2020 ambapo alikutwa na silaha aina ya Pisto.

Shtaka la nne linamkabili pia adam la kupatikana na risasi tatu pasipokuwa na leseni na sla tano linamkabili Halfani la kukutwa na sare na vifaa vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), anadaiwa kutenda kosa hilo tarehe 10 Agosti 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!