May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Diamond amuaga Maulid Kitenge, arejea EFM

Maulid Kitenge

Spread the love

 

MTANGAZAJI maarufu nchini Tanzania wa vipindi vya michezo, Maulid Kitenge leo Ijumaa, tarehe 6 Agosti 2021, amerejea kituo cha Redio cha EFM, akitokea Wasafi Media. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Amerejea tena EFM baada ya kutimka Oktoba mwaka 2019 na kwenda kujiunga na Wasafi Media zote za jijini Dar es Salaam alikokuwa mkuu wa kitengo cha michezo, nafasi aliyokuwa nayo pia EFM.

Kitenge ametambulishwa katika kipindi cha Sport HQ na Mkurugenzi wa EFM, Francis Ciza maarufu Majizo.

Jana usiku Alhamisi, kurasa mbalimbali za Wasafi Media akiwemo Ofisa Mtendaji Mkuu wake, Diamond Platinum ilitoa shukuran kwa Kitenge kwa utumishi wake ndani ya taasisi yao.

Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Maulid Kitenge

Diamond, aliweka picha ya Kitenge akiwa studio za Wasafi na kuandika “kwanza kabisa nikushukuru kwa mchango wako mkubwa katika taasisi ya Wasafi Media, kwa kuwa nasi bega kwa bega kuanzia media changa mpaka leo imekuwa media nambari moja nchini katika kila report.

…hakika haikuwa rahisi, shukran sana na sasa nina amani ukirudi nyumbani…mbali ya ushiriki wako kwenye media, siku zote umekuwa ni kama kaka ama Uncle kwangu…na ninakuahidi kwenda kwa kasi ileile ambayo siku zote umenisihi kuifanya, ili kutimiza malengo ya WASAFI MEDIA kuwa chombo kikubwa cha habari africa na kuzidi kulipa heshima Taifa letu katika nyanja ya habari.”

Kitenge alijiunga na EFM mwaka 2015 akitokea Kampuni ya IPP- Radio One na ITV na kuhudumu EFM kama Mkuu wa Idara ya Vipindi vya Michezo, akitangaza vipindi vya michezo vya Sports Headquarters na E-Sport, pamoja na kusoma magazeti katika Kipindi cha Joto la Asubuhi ndani ya EFM.

error: Content is protected !!