May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NCCR-Mageuzi yajitosa kesi ya Mbowe, kutuma mawakili 5

Spread the love

 

CHAMA cha upinzani nchini Tanzania cha NCCR-Mageuzi, kimesema kitatuma mawakili wake watano waandamizi wakiongozwa na Boniface Mwambukusi, katika kesi ya ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa, tarehe 6 Agosti 2021 na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam alipokwenda kusikiliza kesi hiyo.

Mbatia amesema chama chake kitachukua hatua hiyo, ili kuhakikisha haki inatendeka kwa kuwa kesi hiyo ina maslahi ya Taifa katika uchumi, kisiasa na kijamii.

“Kwa sababu kesi hii ni ya kitaifa, ina maslahi ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kisheria, sisi tumeamua ili haki itendeke tutaweka mawakili kusaidiana na jopo la mawakili wa utetezi.”

Freeman Mbowe akiwa mahakamani Kisutu

“Mawakili wataongozwa na Boniface Mwambukusi na wenzake wanne ambao ni waandamizi, kwa ajili ya kusaidi katika kesi hii kuona haki inatendeka,” amesema Mbatia.

Mbali na Mbowe ambaye ni Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo cha Chadema, wengine ni Halfan Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa na Mohammed Abdillah Lingwenya.

Mbowe na wenzake wamesomewa upya mashtaka matano ikiwemo kupanga njama za ugaidi, kufadhili vitendo hivyo na uhujumu uchumi.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 13 Agosti 2021.

error: Content is protected !!