Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kikosi Kazi: Mikutano ya hadhara iruhusiwe, matokeo ya urais yahojiwe mahakamani
Habari za SiasaTangulizi

Kikosi Kazi: Mikutano ya hadhara iruhusiwe, matokeo ya urais yahojiwe mahakamani

Spread the love

HATIMAYE Kikosi Kazi cha kukusanya maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi nchini Tanzania kilichoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan kimeitimisha kazi hiyo na kupendekeza kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara na kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais mahakamani. Anaripoti Jonas Mushi, Dar es Salaam … (endelea)

Mapendekezo hayo yamewasilishwa kwa Rais Samia leo Ijumaa tarehe 21 Oktoba, 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kiikosi kazi hicho kufanya kazi kwa takribani miezi tisa kikiwa na masuala tisa yaliyohitaji maoni ya wadau.

Akisoma mapendekezo hayo Mwenyekiti wa Kikosi Kazi, Profesa Rwekaza Mkandala, amesema wanapendekeza mikutano ya hadhara na ya ndani ya vyama vya siasa iendelee kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi. Pia imependekeza marekebisho ya baadhi ya vifungu vya Sheria ya Vyama vya Siasa ili mikutano hiyo ifanyike kwa ufanisi.

Itakumbukwa kuwa mikutano ya hadhara ilikatazwa kwa tamko la Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk. John Magufuli pasipo maoni ya wananchi wala wadau wa siasa nchini.

Mbali na mikutano ya hadhara pia kikosi kazi kimependekeza matokeo ya uchaguzi wa Urais yaruhusiwe kuhojiwa katika mahakama ya juu pamoja na kuwawajibisha watendaji wa Tume Huru ya Uchaguzi watakaokiuka sheria na taratibu za uchaguzi ikiwemo kuwaengua wagombea bila kufuata taratibu.

Kwa mujibu wa Ibara ya 41 ibara ndogo ya saba ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ikishamtangaza mshindi wa Urais hakuna mahakama yenye mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake.

Pia kikosi kazi hicho imependekeza utaratibu wa utoaji wa ruzuku uliopo uendelee isipokuwa asilimia 10 ya ruzuku ya vyama vya siasa, igawanywe sawa kwa vyama vyote vya siasa.

Prof. Mukandala amesema vyama vitakavyopewa ruzuku visiwe vimepata hati chafu katika Ukaguzi wa Mdhibiti wa Hesabu za Serikali katika mwaka wa fedha uliopita na viwe vimehakikiwa kama vinakidhi vigezo vya kuwa vyama vya siasa.

Aidha Kikosi kazi kimependeka Sheria ya vyama vya siasa ifanyiwe marekebisho ili kulipatia baraza la vyama vya siasa linaloundwa na vyama vyenyewe mamkali ya kushughulikia suala la uvunjifu wa maadili ya vyama vya siasa kupitia kamati yake ya maadili na Msajili wa Vyama vya siasa aandae muongozo wa chaguzi za ndani za vyama vya siasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!