Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Zimbabwe yawa nchi ya kwanza Afrika kukubali chanjo ya VVU
KimataifaTangulizi

Zimbabwe yawa nchi ya kwanza Afrika kukubali chanjo ya VVU

Spread the love

ZIMBABWE imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika na ya tatu duniani kuidhinisha dawa ya kuzuia VVU iliyopendekezwa hivi karibuni na Shirika la Afya Duniani (WHO). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Wadhibiti nchini Australia na Marekani tayari wameunga mkono kutumia dawa ya muda mrefu ya sindano ya Cabotegravir (CAB-LA), na WHO ilipongeza hatua hiyo ya Zimbabwe.

Dawa ya kuzuia VVU ambayo inaweza kuokoa mamilioni ya watu – ikiwa wanaweza kumudu

Mapambano dhidi ya VVU nchini humo yameshuhudia vifo vinavyohusiana na Ukimwi kupungua kutoka wastani wa 130,000 mwaka 2002 hadi 20,000 mwaka 2021.

Mwaka jana ilizindua mpango mkakati wa kukomesha Ukimwi ifikapo 2030 na tayari imefikia lengo linalojulikana kama 90-90-90 – 90% ya watu wanaoishi na VVU kujua hali zao; 90% kupata matibabu ya kurefusha maisha; na 90% kuwa na virusi visivyoweza kusambaa.

Mfumo wa huduma ya afya wa Zimbabwe unakabiliwa na matatizo makubwa wakati wa mzozo wa kiuchumi wa nchi hiyo.

WHO ilisema katika taarifa kwamba kuidhinishwa kwa udhibiti ni “hatua muhimu”, na kuongeza kuwa itasaidia Zimbabwe “kubuni na kuendeleza programu ili CAB-LA iweze kutekelezwa, kwa usalama na kwa ufanisi, kwa matokeo makubwa”.

Dawa hiyo imeongeza matumaini ya kupunguza zaidi vifo kusini mwa Afrika na inafuata pendekezo la WHO mwezi Julai kwamba CAB-LA ina ufanisi mkubwa katika kupunguza maambukizi miongoni mwa watu walio katika hatari zaidi ya kuambukizwa VVU.

Nyasha Sithole, wa mtandao wa Agenda ya Maendeleo kwa Wasichana na Wanawake barani Afrika (DAWA), alisema: “Kuharakisha uzuiaji wa VVU kwa wasichana na wanawake vijana kunahitaji upanuzi wa njia zilizopo.

Ninafurahi na kujivunia kujua kwamba nchi yangu imeidhinisha matumizi ya CAB-LA. Hii itachangia kapu letu la zana za kuzuia VVU ambazo zinafanya kazi kwetu kama wasichana na wanawake nchini Zimbabwe.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

error: Content is protected !!