Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Watanzania wamegawanyika kuhusu Katiba: Kikosi Kazi
Habari za Siasa

Watanzania wamegawanyika kuhusu Katiba: Kikosi Kazi

Profesa Rwekaza Mukandala
Spread the love

TOFAUTI na masuala mengine yaliyofanyiwa kazi na Kikosi Kazi cha kukusanya maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi, suala la Katiba limetajwa kuwa na maoni tofauti ya wananchi jambo linaloonesha namna suala hilo lilivyo na ugumu. Anaripoti Jonas Mushi, Dar es Salaam … (endelea)

Hata hivyo Kikosi Kazi hicho kimetoa maoni ya namna ya kuondokana na mkwamo uliopo wa Katiba Pendekezwa ambayo ilikwama baada ya mgawanyiko wa vyama vya siasa katika Bunge Maalum la Katiba na kushindwa kwenda kwenye hatua nyingine ya kupigiwa kura ya maoni.

Mwenyekiti wa Kikosi Kazi, Profesa Rwekaza Mkandala amesema Watanzania wamegawanyika katika makundi mawili wakiwemo wanaotaka marekebisho ya katiba iliyopo na wale wanaotaka kuwepo kwa Katiba mpya.

Aidha amesema watanzania wamegawanyika katika makundi matano kuhusu njia ya kupata katiba mpya wakiwemo wanaopendekeza mchakato kuanza upya na kwamba utekelezaji wa mchakato huo unahitaji muda na gharama.

Amesema baadhi ya wadau walipendekeza kuwa mchakato uendelee pale ulipoishia na kwamba mtazamo huo ungeweza kupunguza gharama lakini una changamoto kwamba ni takribani miaka minane tangu Katiba inayopendekezwa upitishwe na kwamba huenda ukawa umepitwa na wakati.

https://www.youtube.com/watch?v=swGH512xibw&t=806s

“Wapo waliopendekeza Katiba i=pendekezwa ifanyiwe marekebisho ili iendane na wakati uliopo aidha tangu ipatikane kumefanyika uchaguzi mara mbili… ambazo zimetoa uzoefu wa aina mbalimbali unaoweza kuboresha Katiba Pendekezwa,” amesema.

Ameongeza kuwa baadhi ya wadau walipendekeza kuwa mchakato uendelee katika rasimu ya opili ya Katiba na kwamba mtazamo huo hautekelezekeki kwani unakiuka utaratibu ulioanishwa na Sheria ya mabadiliko ya KAtiba ambayo inaelekeza rasimu hiyokuwasilishw akatika Bunge maalum la Katiba.

Prof. Makandala amebainisha kuwa baadhi ya wadau walipendekeza kuundwa kwa jopo la wataalam ili kuoanisha Katiba iliyopendekezwa na Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya ili kupunguza gharama na kwamba jopo hilo liandae rasimu mpya.

Aidha amesema wapo waliosema hakuna haja ya katiba mpya bali katiba iliyopo ifanyiwe marekebisho ili iendane na wakati uliopo.

Prof,. Mkandala amesema baada ya kupokea maoni hayo Kikosi Kazi kimekuja na mapendekezo ya hatua za kupata Katiba mpya ikiwemo mjadala wa kitaifa kuhusu masuala ya msingi, kuhuisha Sheria ya Katiba Mpya na Sheria ya Kura ya maoni, kuundwa kwa jopo la wataalamu watakaounda rasimu ya katiba, Rasimu kupitishwa na Bunge, elimu ya uraia kwa wananchi na kura ya maoni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!