Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kero 22 kati ya 25 za Muungano zapatiwa ufumbuzi
Habari za Siasa

Kero 22 kati ya 25 za Muungano zapatiwa ufumbuzi

Spread the love

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dk. Selemani Jafo amesema tangu kuanzishwa kwa Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) mwaka 2006, hoja 25 zimejadiliwa na kati ya hizo 22 tayari zimepatiwa na kuondolewa kwenye hoja za muungano. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Dk. Jafo ametoa kauli hiyo leo Ijumaa bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Najma Murtaza Giga (CCM) aliyetaka kujua mikakati ya Serikali ya kuhakikisha changamoto za Muungano ambazo hazijapatiwa ufumbuzi hazileti madhara nchini na lini zitapatiwa ufumbuzi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dk. Selemani Jafo.

Akiendelea kujibu swali hilo, Dk. Jafo amesema SJMT na SMZ zimetengeneza utaratibu wa kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali za Muungano kupitia vikao vyake.

Amesema kuwa Serikali hizo mbili ziliunda Kamati ya Pamoja ya kutatua changamoto za Muungano ambayo huundwa na wajumbe kutoka pande zote mbili za Muungano.

Aidha, ameongeza kuwa hoja mbili zilizobaki katika orodha hiyo zipo katika hatua za kupatiwa ufumbuzi kupitia kamati hiyo inayoundwa na wajumbe kutoka SJMT na SMZ.

Aidha, Dk. Jafo amesisitiza kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali inayoongozwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi wana nia ya dhati ya kuzitafutia ufumbuzi hoja hizo mbili zilizobaki.

Kwa upande Giga ametoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutatua changamoto za Muungano na kuonesha imani kuwa zilizobaki zitatafutiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!