February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kangi Lugola: Mwananchi akifia kwenye mapenzi kachomeni kitanda

Kangi Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

Spread the love

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameshangazwa na kitendo cha baadhi ya wananchi kuchoma vituo vya polisi pindi raia anapofariki mikononi mwa polisi, na kuhoji kuwa, kwanini mtu akifariki wakati anafanya mapenzi hawachomi kitanda cha gesti. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Waziri Lugola ameyahoji hayo leo tarehe 13 Septemba 2018 bungeni jijini Dodoma wakati akitoa kauli ya serikali kuhusu watu wanaodaiwa kufia mikononi mwa vyombo vya dola.

“Mtu akifa polisi wananchi huchoma vituo vya polisi. Mtu akifa wakati anafanya mapenzi mbona wananchi hawaendi kuchomba kitanda?” amehoji Waziri Lugola.

Akifafanua kuhusu utokeaji wa matukio ya raia kuuawa mikononi mwa polisi, Waziri Lugola amesema kuwa, mtu hufa wakati wowote na mahali popote na hivyo si ajabu mwananchi kufia polisi, ingawa amekiri uwepo wa matukio hayo na kusema kuwa, serikali inafanya uchunguzi na kuwachukulia hatua wahusika wanapothibitika kusababisha kifo hicho.

“Mwananchi kufa anakufa wakati wowote ,mahali popote ndio maana kwenye biblia,imeandikwa kifo ni mtego humnasa mtu wakati wowote mahali popote, hivyo mwananchi anaweza akafa akiwa polisi, akiwa anafanya mapenzi, au kwenye gari, msifikirie anayefia polisi ni kwamba anateswa, lakini nakiri kuna matukio ya raia kufia polisi na tunachukua hatua baada ya uchunguzi kufanyika,” amesema.

error: Content is protected !!