Friday , 2 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Waliokutwa na madini kinyume na sheria, wakwepa kifungo
Habari Mchanganyiko

Waliokutwa na madini kinyume na sheria, wakwepa kifungo

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu miaka mitatu jela ama kulipa faini ya Sh. 24 milioni wafanyabiashara wawili wa madini baada ya kukiri kosa la kukutwa na madini ya Coloured Gemstones yenye thamani ya Dola za Kimarekani 1.8 milioni. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Pia mahakama hiyo imeamuru madini hayo yataifishwe. Hata hivyo, washtakiwa hao wameweza kuepuka kutumikia kifungo hicho baada ya kulipa faini hiyo.

Hukumu hiyo, imetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwizire baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Joseph Pande kuwasomea mashtaka mawili washtakiwa hao ambapo walikiri makosa yao.

Baada ya kukiri makosa yao, Mahakama iliradhimika kuhamia maeneo ya Msasani Kinondoni Dar es Salaam ambapo vielelezo vya kesi hiyo vilikuwepo, ambapo kesi iliendeshwa na washtakiwa kutiwa hatiani. Washitakiwa hao ni Aazam Nazim (Raia wa India) na Ango Mbossa raia wa Tanzania.

Hakimu Rwizire hivyo alimtaka kila mshtakiwa kulipa faini ya Sh. 6 milioni kwa kila kosa ama kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela katika kila kosa.

Kwa kuwa kila mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka mawili hivyo kila mshtakiwa atapaswa kutoa faini ya Sh. 12 milioni iwapo atashindwa atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela kwa kuwa vifungo hivyo vinaenda sambamba.

Washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa yao kati ya January 2017 na June 2018 katika maeneo ya Misisiri A eneo la Mwananyamala.

Wanadaiwa kukutwa na madini aina ya Coloured Gemstones kilogramu 75,920.04 yenye thamani
ya Dola za Kimarekani 1,795,687.87.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

Habari Mchanganyiko

Dk. Gwajima atoa maelekezo kwa maofisa maendeleo nchini

Spread the love  WAZIRI wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto,...

error: Content is protected !!