Thursday , 13 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Spika Ndugai azuia wakurugenzi wa Uchaguzi kuguswa
Habari za Siasa

Spika Ndugai azuia wakurugenzi wa Uchaguzi kuguswa

Spread the love

SPIKA wa Bunge Job Ndugai amemzuia Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Susan Kolimba kujibu maswali ya Mbunge wa Kitambile Masoud Abdallah Salim ambapo mojawapo lilihoji kuwa, lini serikali itapeleka mswada bungeni wa kubadili sheria inayoruhusu Wakurugenzi wa Halmashauri kuwa wasimamizi wa uchaguzi. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Salim aliuliza amswali hayo leo tarehe 13 Septemba 2018 bungeni jijini Dodoma, ambapo amedai kuwa, kitendo cha wakurugenzi wa halmashauri kuwa wasimamizi wa uchaguzi, kinaminya uhuru wa demokrasia kutokana kwamba wakurugenzi hao ni makada wa chama tawala nchini CCM na hivyo ikifika kipindi cha uchaguzi wanakuwa marefa wa kuisaidia CCM kupata ushindi.

Mbunge huyo alilielekeza maswali mawili ya nyongeza katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ambapo swali lilingine aliihoji wizara hiyo kwamba, kwa nini serikali imeshindwa kudhibiti mfumuko wa bei ya sukari kitendo kinachochangia ugumu wa maisha kwa wananchi.

Baada ya Salim kuuliza maswali hayo, Spika Ndugai aliyakataa maswali hayo akisema kuwa hayaendani na swali lake la msingi pamoja na kuuliza katika wizara isiyo sahihi, lakini pia kuhusu swali lake mfumuko wa bei ya sukari, alisema litajibiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

IFP wakubali kuungana na ANC kuunda serikali

Spread the loveChama cha upinzani nchini Afrika Kusini, Inkatha Freedom Party (IFP)...

BiasharaHabari za Siasa

Prof. Mkumbo: Pato la taifa limefikia trilioni 148

Spread the loveWaziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema mwaka...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Deni la Serikali lafikia trilioni 91

Spread the loveWaziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Mbunge Dk. Shogo Mlozi afariki dunia

Spread the loveMbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) ambaye pia ni...

error: Content is protected !!