KAMPUNI ya Mkwama imejitosa katika ununuzi wa zao la tumbaku mkoani Tabora na kuwataka wakulima wa mkoa huo kulima kwa wingi zao hilo kwa sababu sasa soko lipo la uhakika. Anaripoti Paul Kayanda, Tabora … (endelea).
Kampuni hiyo imetamba kuwa imejipanga katika ushindani wa masoko na tumbaku yote itanunuliwa.
Hayo yameelezwa jana tarehe 25 Aprili 2023 na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Ahmed Mansoor Huwel wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Tabora baada ya uzinduzi wa masoko ya tumbaku kwenye maghala yake yaliyozinduliwa na mkuu wa mkoa wa Tabora, Balozi Dk. Batilda Burian.
Aidha, alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuikaribisha kampuni hiyo ya mzawa kwenye sekta ya tumbaku huku Waziri wa Kilimo, Husein Bashe akiwapa nguvu wanunuzi wa zao hilo ili kuwasaidia wakulima hao.
Alisema kuwa ili kuendelea kusaidia na kunyanyua wakulima wametumia zaidi ya Sh milion 45 kufufua na kuwasha kiwanda cha tumbaku Morogoro licha ya kwamba mwaka jana walikuwa wageni katika biashara hiyo.
“Nachotaka kusema wakulima wote warudi waende mashambani Mkwawa tumejipanga vizuri, masoko ni yakutosha kwa hiyo tutashawishi wakulima kurudi mashambani na niombe sana kwa walioacha kulima tumbaku warudi kampuni yao ya mzawa imerudi nyumbani kukomboa wakulima,” alisema.
Leave a comment