Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kakoso: Bandari Karema haina maana bila reli, barabara
Habari za Siasa

Kakoso: Bandari Karema haina maana bila reli, barabara

Spread the love

MBUNGE wa Mpanda Vijijini, Selemani Kakoso (CCM) amesema mradi wa wa ujnenzi wa Bandari ya Karema katika Ziwa Tanganyika hautakuwa na maana kama hautaunganishwa na reli na barabara nzuri. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Ameyasema hayo leo Jumatatu ya terehe 11 Aprili, 2022 bungeni jijini Dodoma alipokuwa akichangia hoja bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara zake .

Kakoso ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu amesema ni vyema unejzi wa bandari hiyo kwenda sambamba na ujenzi wa reli kutoka Kaliua-Mpanda hadi Karema.

Amesema pia lazima kuwe na mpango uwekezaji katika ujenzi wa barabara ya Kabungu hadi Karema ili kuiunganisha bandari hiyo na bandari ya Dar es Salaam.

“Tunayo fursa ambayo tunaweza kuipata Serikali ikiwekeza inavyopaswa. Sisi kama nchi ni vyema tukawa na uwekezaji mkubwa ili wananchi wanufaike.

“Tujipange kuahakikisha nchi ya DRC ambayo imejiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki, inatumia ile bandari na ikunganishwa na matawi ya reli na barabara tuna fursa kubwa ya bandari ya Dar es Salaam kupata mzigo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!