Thursday , 2 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge aitaka Serikali ianzishe kilimo cha makambi
Habari za Siasa

Mbunge aitaka Serikali ianzishe kilimo cha makambi

Spread the love

MBUNGE wa Bukoba Vijijini, Dk. Jasson Rweikiza ameishauri Serikali kuanzisha utaratibu wa kilimo cha makambi ili kuongeza uzalishaji mali na ajira kwa vijana. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Dk. Rweikiza ametoa wito huo leo Jumatatu tarehe 11 Aprili, 2022, bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hoja ya hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara zake.

Amesema kupitia makambi hayo Serikali itoe mikopo itakayowawezesha kujenga kambi, kununua trekta, na pembejeo zingine za kilimo.

“Mfano tukianzisha kambi za vijana 200, wapewe hekari 2000 na mkopo wa milioni 200 waanze na mazao ya muda mfupi mfano maharage, mahindi, alizeti n.k baadaya miezi mitatu watapata mazao mengi na watauza nje,” amesema.

Amesema baada ya mwaka mmoja kama watakuwa wanafanya kilimo cha umwagiliaji, wataweza kurejesha mkopo wao na wataendelea na uzalishaji, “wanaweza wakajilipa mishahara ya milioni moja kila mwezi na tukaondokana na tatizo la ajira.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kamati ya Bunge yaitaka Serikali ichukue hatua kudhibiti mfumuko wa bei

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania imetakiwa kufanya tathimini dhidi ya changamoto...

Habari za Siasa

Bunge lataja kinachokwamisha Mradi wa Mchuchuma na Liganga

Spread the love  MRADI wa uchimbaji chuma cha Liganga na Makaa ya...

Habari za Siasa

Chongolo aagiza watendaji wanaoonyesha mianya ya rushwa wakamatwe

Spread the love   KATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa...

Habari za Siasa

TRA iweke mfumo wa msamaha wa kodi kutekeleza miradi

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kimeitaka Mamlaka ya Mapato...

error: Content is protected !!