Tuesday , 30 May 2023
Home Habari Mchanganyiko JPM: Ole wako Mufti uoe mke mwingine
Habari MchanganyikoTangulizi

JPM: Ole wako Mufti uoe mke mwingine

Spread the love

RAIS John Magufuli amemkabidhi Sh. 10 Mil Mufti wa Tanzania, Aboubakar Bin Zubeir kwa ajili ya kusaidia kuendeleza Qur’an nchini. Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Akimkabidhi fedha hizo Rais Magufuli amesema, amempa fedha hizo si kwa ajili ya kwenda kuoa mke mwingine bali uendeleza Qur’an kwa Waislam na wasio Waislam.

Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 19 Mei 2019, wakati wa Mashindano ya 20 ya Kuhifadhi na Kusoma Qur’an Afrika, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa wa Mpira jijini Dar es Salaam.

“Mufti nawe nitakupa zawadi ya shilingi milioni 10, ole wako ukaongeze mke mwingine. Hawa watani zangu, mtu wa Pwani ukimpa fedha anakwenda kuoa hahahaaa,” amesema.

Katika mashindano hayo, mshindi wa kwanza ametajwa kuwa ni Mohammed Dialo kutoka nchini Senegal ambaye amekabidhiwa kitita cha Sh. 20. Mil pamoja na tiketi ya kwenda Hijja.

Mshindi wa pili ni Farouq Yaqub kutoka Nigeria ambaye amepewa zawadi ya Sh. 12 Mil, mshindi wa tatu ni Shamsudin Hussein Ali kutoka visiwani Zanzibar, Tanzania aliyejinyakulia Sh. 70 Mil.

Mshindi wa nne ametajwa kutoka Niger, Idris Othman ambaye amepata zawadi ya Sh. 5 Mil na mshindi wa tano ametoka Tanzania ambaye ni Sumaiya Juma Abddallah aliyezawadiwa Sh. 3 Mil huku Rais Magufuli akimwongezea Sh. 1 Mil kwa kuwa, ndio mtoto wa kike pekee kati ya washiriki 20.

Mashindano hayo yameyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwemo Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu; Ali Hasaan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili; Dk. Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne; Gharib Bilali, Makamu wa Rais Mstaafu na viongozi wengine wa kitaifa na kimataifa.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemaliza utata wa kupatikana kwa eneo lililopo katika Manispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam lililokuwa likiombwa na Taasisi Al-Hikma Foundation kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya.

Rais Magufuli amesema, eneo hilo kwa kuwa litatumika kwa ajili ya huduma za kijamii, anaziagiza mamlaka husika kuhakikisha eneo hilo linakabidhiwa taasisi hiyo ndani ya wiki moja.

“Najua eneo mnalolitaka ni eneo la wazi, lakini kwa sasa linatupiwa uchagu. Kama ni hivyo, kwanini nisilitoe kwa ajili ya huduma hiyo. Nitoe rai kwamba, eneo hilo nitalifuatilia ili kuona kama limetumika kikamilifu,” amesema Rais Magufuli.

Ombi la eneo hilo lilitolewa na Sheikh Nurdin Kish, Msimaizi wa mashindano hayo kwamba, wamekuwa wakihangaika kufuata taratibu zole lakini wamekuwa wakikumbana na vikwazo.

Akizungumzauanzishwaji wa mashindano hayo, Sheikh Kish amesema kuwa, yalianzishwa mwaka 2000 na kwamba, sasa mashindano hayo yanatimiza miaka 20.

Pia amemshukuru Rais Magufuli wa kutenga muda wake na kujumuika kwenye mashindano hayo, licha ya kuwa na majukumu mengi.

“Mheshimiwa rais, kwa unyenyekevu wako na upendo wa hali ya juu, kwa wingi wa mambo ambayo unayo, tulikuomba uje mwishoni mwishoni walau upate kusikiliza washiriki wa mwisho, lakini ukaona uje mapema, umetupa heshima kubwa,” amesema Sheikh Nurdin.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wenye ulemavu waiomba MISA-TAN iwajengee uwezo wa uhuru wa kujieleza

Spread the love  TAASISI ya vyombo vya Habari kusini mwa Afrika (MISA-TAN)...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wajawazito 2000 Korogwe washiriki Marathon, Mwenyekiti UWT amsifu Jokate

Spread the loveWANAWAKE wajawazito zaidi ya 2000 wilayani Korogwe mkoani Tanga wameshiriki...

Habari Mchanganyiko

Kirigini kuzikwa leo Butiama

Spread the love  MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Musoma Vijijini (1980-1985), Herman...

Habari za SiasaTangulizi

Uamuzi juu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi 13 Juni

Spread the love  MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR), imepanga...

error: Content is protected !!