Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kiongozi wa Mwenge: Mwanza inatekeleza miradi kwa kiwango bora
Habari Mchanganyiko

Kiongozi wa Mwenge: Mwanza inatekeleza miradi kwa kiwango bora

Mzee Mkongea Ali, Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa
Spread the love

MZEE Mkongea Ali, Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa, amesema miradi ya maendeleo ikiwemo ya maji na shule inayoendelea kutekelezwa katika Jiji la Mwanza ni miongoni mwa miradi bora na yenye kiwango cha hali ya juu. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Mkongea ametoa kauli hiyo jana wakati akizindua, kufungua na uwekaji jiwe la msingi katika miradi 10 yenye thamani ya zaidi Sh. 4 bilioni katika Halmashauri ya jiji la Mwanza. 

Miradi aliyopita na kupongeza utekelezaji wake ni pamoja na zahanati ya kisasa ya Mhandu iliyogharimu zaidi ya Sh. 100 milioni, mradi wa usambazaji maji Lwanima unaogharimu zaidi ya Sh. 2 bilioni, mradi wa tofali eneo la Buhongwa, ujenzi wa vyumba vya madarasa Buhongwa A na B.

Miradi mingine ni ujenzi wa vyumba viwili na vya kisasa shule ya msingi Igoma, eneo alipopumzika Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere baada ya kutembea kwa mguu kutoka Butiama, pamoja na kukabidhi hundi ya Sh. 10 milioni kwa wajasiliamali eneo la Makoroboi.

Akizungumza katika mradi wa maji wa Lwanima, kiongozi huyo wa mbio za Mwenge, alisema maeneo mengi walikopita wamekuta miradi mingi ikitekelezwa chini ya kiwango lakini hali hiyo hajaiona katika Jiji la Mwanza.

Alisema kuwa miradi mingi ambayo inasimamiwa na wahandisi wanaume katika baadhi ya halmashauri imekuwana na changamoto nyingi ikiwemo kutekelezwa chini ya kiwango.

“Maeneo ambayo tumepita tumekutana na wahandisi wanaume na ambao wanasimamia miradi ukiangalia mingi ni mibovu tena na wengine hata ukiomba taarifa za kina na sahihi hazipo lakini kwa Jiji la Mwanza mnajitahidi sana.

“Labda ambacho nimebaini hapa jijini Mwanza ni kutokana na miradi mikubwa yote na ile ya muhimu wasimamizi wake ni wahandisi wa kike ambao usimamizi wao ni mzuri, hongereni na endeleeni hivyo hivyo,” alisema Mkongea.

Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge ambaye alianza ziara yake jana saa 10:43, alipofika katika mradi wa tano ule wa usambazaji wa maji, alisema kila miradi ya jiji anakopita inatia matumaini hivyo hana sababu ya kuendelea kukagua.

“Miradi yenu ni mizuri sana yaani hapa hata kasi yangu ya kukagua nimeipunguza ukilinganisha na wilaya nyingine ambazo tumepita hali ni mbaya, mkurugenzi Jiji (Kiomoni Kibamba) na mkuu wa wilaya mnafanya kazi nzuri,” alisema Mkongea.

Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba alisema kazi kubwa iliyomleta Mwanza ni kufanya kazi na kusimamia fedha ya umma ili kuhakikisha inafanya kazi iliyokusudiwa.

“Mimi kuongea kwangu ni kuonyesha miradi kama hii ambayo inajieleza yenyewe na hii ndio mipango yangu kuhakikisha kwa muda ambao nitakaokuwa hapa miradi mingi itekelezeke,” alisema Kibamba.

Mhandisi wa maji Jiji la Mwanza, Godliver Gwambasa alisema mradi huo unatarajiwa kukamilika Juni mwaka huu na kazi iliyobaki ni ndogo kwani pambu na bomba zote zimenunuliwa na tayari zimeanza kufungwa.

“Mradi upo kwenye asilimia 80 za utekelezaji wake, kilichobaki ni fedha zile ambazo tumeziomba Serikali Kuu kuja ili kumalizia kazi iliyobaki kama kukamilisha nyumba za walinzi na kulipa Sh. 388 milioni ambazo tunadaiwa na mkandarasi wa mradi,” alisema Mhandisi Gwambasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

error: Content is protected !!