Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa JPM atengua Ma-DC, RAS, DED na RC akiwemo Makonda
Habari za SiasaTangulizi

JPM atengua Ma-DC, RAS, DED na RC akiwemo Makonda

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa mikoa (RC), Wakuu wa Wilaya (DC), Katibu Tawala wa Mikoa (RAS) na Wakurugenzi wa Halmashauri (DED). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema, Kwanza, Rais Magufuli amemteua Aboubakar Kunenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Kabla ya uteuzi huo, Kunenge alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Paul Christian Makonda.

Aboubakar Kunenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Pili, Rais Magufuli amemteua Joseph Mkirikiti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

Kabla ya uteuzi huo, Mkirikiti alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mkoa wa Manyara na anachukua nafasi ya Alexander Pastory Mnyeti.

Tatu, Rais Magufuli amemteua Paulo Mshimo Makanza kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Kabla ya uteuzi huo, Makanza alikuwa Afisa Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na anachukua nafasi ya Kunenge ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Nne, Rais Magufuli amemteua Dk. Seleman Serera kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma.

Kabla ya uteuzi huo Dk. Serera alikuwa Afisa Mwandamizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Makao Makuu na anachukua nafasi ya Deo Ndejembi.

Tano, Rais Magufuli amemteua Ssgt. Mayeka Simon Mayeka kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya.

Kabla ya uteuzi huo, Ssgt. Mayeka alikuwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na anachukua nafasi ya MarryPrisca Makundi.

Soma zaidi..

Sita, Rais Magufuli amemteua Kanali Patrick Norbert Songea kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara.

Kabla ya uteuzi huo, Kanali Songea alikuwa Afisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na anachukua nafasi ya Tumaini Magesa.

Saba, Rais Magufuli amemteua Alhaji Rajab Kundya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro.

Kabla ya uteuzi huo, Alhaji Kundya alikuwa Afisa katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Makao Makuu na anachukua nafasi ya Kippi Warioba.

Nane, Rais Magufuli amemteua Joseph Kashushura Rwiza kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mkoa wa Kigoma.

Kabla ya uteuzi huo, Rwiza alikuwa Afisa Mipango katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Mkoa wa Tabora na anachukua nafasi ya Mhandisi Godfrey Msongwe Kasekenya.

Tisa, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Gharib Lingo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara.

Kabla ya uteuzi huo, Lingo alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma.

Kumi, Rais Magufuli amemteua Frank Fabian Chonya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi.

Kabla ya uteuzi huo, Chonya alikuwa Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi na anachukua nafasi ya Andrea Godfrey Chezue.

Wakati huo huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kepteni mstaafu, George Huruma Mkuchika, kwa mamlaka aliyokasimiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Wilaya kama ifuatavyo;

Kwanza, amemteua Juvenile Jaka Mwambi kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Tandahimba Mkoa wa Mtwara.

Juvenile Jaka Mwambi anachukua nafasi ya Benaya Liuka Kapinga.

Pili, amemteua Mashaka Boniface Mgeta kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga.

Mgeta anachukua nafasi ya Boniface Maiga aliyefariki dunia hivi karibuni.

Tatu, amemteua Johari Khamis Athuman kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjaro.

Johari Khamis Athuman alikuwa Afisa katika Ofisi ya Rais na anachukua nafasi ya Aboubakar Asenga.

Nne, amemteua Ayoub Amir Perro kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi.

Kabla ya uteuzi huo, Perro alikuwa Afisa katika Ofisi ya Upelelezi ya Polisi Mkoa wa Kigoma na anachukua nafasi ya Twaha A. Mpembenwe.

“Wateule wote wawepo Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma kesho Alhamisi tarehe 16 Julai, 2020 saa 4:00 asubuhi,” amesema Msigwa

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!