Monday , 22 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Magufuli asalimu amri kwa wafanyakazi
Habari za SiasaTangulizi

Magufuli asalimu amri kwa wafanyakazi

Rais John Magufuli
Spread the love
HATIMAYE Rais John Pombe Magufuli, amesikia kilio cha wafanyakazi nchini. Amefuta angalau kwa muda, matumizi ya kanuni mpya ya kikokotoo cha mafao ya wastaafu nchini.Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kabla ya tangazo hilo la rais, kikokotoo kilikuwa kinawaelekeza wastaafu kulipwa asimilia 25 ya mafao yao mara wanapostaafu na asilimia 75 inayobakia, kulipwa kila mwezi.

Akizungumza na viongozi wa vyama vya wafanyakazi na mamlaka inayosimamia mifuko ya hifadhi ya jamii, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Ijumaa, rais aliagiza kusitishwa kanuni mpya na kuruhusu kuendelea kutumika kwa kanuni za zamani hadi mwaka 2023.

Ametaka mamlaka husika kuhakikisha wastaafu wanalipwa kikokotoo kilichokuwa kinatumika kabla mifuko hiyo kuunganishwa ambacho ni asilimia 50, hadi pale serikali itakapounda mfumo mpya wa malipo ya mafao.

Januari mwaka huu, Bunge lilipitisha sheria ya mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma na baadaye waziri mwenye dhamana ya masuala ya kazi, Jenista Mhagama, aliunda kanuni hiyo mpya iliyopingwa na wafanyakazi wote nchini.

“Mazungumzo yenu yote nimeyasikia. Nimeona angalau tuwe na kipindi cha mpito. Kile kikokotoo kilichokuwa kinatumika kwa kila mfuko kabla ya mifuko kuunganishwa, yaani mfuko wa PSSF, GEPF, LAPF, PPF na NSSF, kiendelee kutumika katika kipindi hiki cha mpito hadi mwaka 2023,” alieleza.

Alisema, “hii maana yake ni kwamba, wastaafu wataendelea kwenye kikotoo cha asilimia 50. Nimepiga hesabu kufka 2023, watakuwa wastaafu 54,000 kwa serikali hii; na katika kipindi hicho hatutashindwa kuwalipa.”

Rais Magufuli alisema, ni matumaini yake kuwa katika kipindi hicho, michango itaendelea kukusanywa na matumizi ya mifuko itapunguzwa na hivyo mifuko hiyo kuimarika.

Aidha, rais amesema katika kipindi hicho cha mpito, kama mifuko hiyo itakuwa imeimarika na michango kuwasilishwa kama inavyotakiwa kikokotoo hicho kinaweza kupandishwa.

Amesema, “tukikuta mifuko imeimarika hata watu wakisema tulipe asilimia 70 haitakua tatizo, hata kama mtu akisema anataka asilimia 100 atalipwa. Nia yangu sio mifuko ife, nataka serikali ipange fomula kwa kushirikiana na mimi, nitashangaa hadi ikifika 2023 hamtapa fomula nzuri.”

Ameongeza, “…kustaafu sio dhambi.  Anayestaafu  anatakiwa kuheshimika, kwa sababu amejitoa kwa ajili ya taifa hili. Huyu ni shujaa na kustaafu bila kufukuzwa, ni heshima. Nina uhakika waziri atahakikisha mifuko haitumiki ovyo.”

Tangu kutungwa kwa kanuni hiyo ya kikokotoo, kumekuwa na manung’uniko kila pembe ya nchi, kulalamikia utaratibu huo ambao unaonekana umelenga kuwapunja wafanyakazi wa sekta za umma na binafsi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

Habari za Siasa

Makamba ataja maeneo ya kuboresha mambo ya nje

Spread the love  WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika...

error: Content is protected !!