February 24, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Jicho la Rais Magufuli lahamia kwa wastaafu hewa

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS John Magufuli amewataka watendaji katika mifuko ya hifadhi ya jamii kuboresha daftari la orodha ya majina ya wastaafu, ili kuondoa mapungufu yaliyopo pamoja na kudhibiti uwepo wa wastaafu hewa. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Dk. Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 28 Desemba 2018 wakati akizungumza na viongozi wa vyama vya wafanyakazi na mifuko ya hifadhi ya jamii, akisema kuwa kama serikali iliwahi kubaini juu ya uwepo wafanyakazi, wanafunzi, mishahara na pembejeo hewa, haiwezi kukosa wastaafu hewa.

“Niwaombe, kwenye mifuko sababu katika mifuko hii waboreshe daftari la wastaafu ili kuondoa wastaafu hewa au usajili wa kujirudia,  kama tumekuwa na wastaafu hewa, pembejeo hewa mishahara hewa, wanafunzi hewa, hatuwezi tukakosa wastaafu hewa, lazima tunao. Hatuwezi tukakosa wastaafu ambao wameandikwa majina mara mbili,” amesema Rais Magufuli.

Katika agizo lingine, Rais Magufuli ameitaka mifuko ya hifadhi ya jamii kupunguza matumizi ya ovyo pamoja na uwekezaji wa miradi isiyo na tija, ili iwe na uwezo wa kulipa mafao ya wastaafu kwa wakati na kiwango kinachotakiwa.

“Mnafahamu hata mifuko hii ilikuwa inaendeshwa kiajabu, pakawa panaanzishwa miradi ya ajabu ajabu na mingi ilikuwa ya majengo, nenda kigamboni uangalie majengo yaliyojengwa, fikiria aliyeweka mabilioni ya fedha alitegemea ataingiza kiasi gani.

“Sina uhakika kama mlikuwa mnaamua mnataka miradi ya aina hii, walikuwa wanaamua watendaji pasipo kushirikisha wafanyakazi,” amesema na kuongeza Rais Magufuli.

“Uwekezaji usio na tija usifanyike,  tupunge gharama za uendeshaji wa mifuko, sababu sasa hivi imebaki mifuko mwili hakuna sababu za kushindana, huu ni mfuko wa sekta binafsi na huu wa umma ina wanachama wake,

error: Content is protected !!