Friday , 1 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa JPM amewataka Watanzania kuvumiliana
Habari za Siasa

JPM amewataka Watanzania kuvumiliana

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS John Magufuli, rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka Watanzania kuwa na mioyo ya kuvumiliana, anaandika Hellen Sisya.

Rais Magufuli ameyasema hayo mapema leo hii akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Singida na kusisitiza kuwa kila mmoja anatakiwa kuilinda amani.

“Niwaombe Watanzania, tuwe na mioyo ya kuvumiliana, tuitunze amani yetu.” alisema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amesisitiza kuwa suala la kulinda amani ni kila mmoja wetu na kuwataka watanzania kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake.

Kauli ya Rais Magufuli imekuja wakati ambao viongozi wa kisiasa wa kambi ya upinzani wakikamatwa mara kwa mara kwa madai ya kutoa lugha za uchochezi, hatua inayoonyesha kuwa bado hakuna uvumilivu wa kisiasa hapa nchini.

Rais Magufuli amekuwa katika ziara ya kikazi kwa siku kadhaa sasa akitembelea mikoa mbalimbali ikiwemo Kigoma, Tabora na leo ndiyo alikuwa anahitimisha ziara hizo mkoani Singida.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari za Siasa

Waziri mkuu Ethiopia atua Tanzania

Spread the loveWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,...

Habari za Siasa

Babu Owino: Vijana msibaki nyuma

Spread the loveMbunge wa Embakasi Mashariki nchini Kenya, Paul Ongili Owino maarafu...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia: Hatutazuia watu kuingia barabarani

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali itaendelea kuruhusu vyama...

error: Content is protected !!