Friday , 1 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Fatma Karume naye amvaa Rais Magufuli
Habari za SiasaTangulizi

Fatma Karume naye amvaa Rais Magufuli

Fatuma Karume, Wakili wa kujitegemea. Picha ndogo Rais John Magufuli
Spread the love

FATUMA Karume, wakili wa Tundu Lissu, Mwanasheria mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema kila mtu ana haki ya kumkosoa Rais, anaandika Hellen Sisya.

Wakili huyo ameyasema hayo nje ya Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu ambapo Lissu amefikishwa siku ya leo akishtakiwa kwa kosa la kutoa lugha ya uchochezi ambayo imeleta chuki katika jamii.

“Kinyago ulichokichonga mwenyewe kweli kikutishe? Maana tukumbuke mwaka 2015, Rais John Pombe Magufuli kaja kutuomba sisi kura.

Kwa hivyo sisi tuna haki leo ya kumkosoa, na hiyo haki tutaipigania.” amesema wakili huyo.
Aidha, wakili huyo alisisitiza kuwa lengo lao lilikuwa ni mteja wao kufikishwa mahakamani, na hilo limetimia.

Hivyo kuwataka wananchi kusubiri hiyo tarehe 27 ambapo uamuzi kuhusu dhamana ya mteja wake utatolewa.

Katika kesi hiyo Mawakili wa upande wa jamhuri walitoa hoja za kupinga dhamana ya Lissu, ambapo mahakama imesema kuwa itatoa uamuzi kuhusiana na dhamana hiyo kesho kutwa hivyo kusababisha Lissu kurejeshwa rumande.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mwili wa Hayati Mwinyi kuagwa leo saa 8 Uwanja wa Uhuru

Spread the loveMWILI wa Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi unatarajiwa kuagwa kuanza...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari za Siasa

Waziri mkuu Ethiopia atua Tanzania

Spread the loveWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,...

error: Content is protected !!