September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

JK awakaribisha wanafunzi UDSM, autega uongozi Dar

Spread the love

JAKAYA Kikwete, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) nchini Tanzania, amewakaribisha wanafunzi wa chuo hicho kuendelea na masomo. Anaripoti Mwandishi wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Kikwete ambaye pia ni Rais mstaafu wa Tanzania, amesema hayo leo Alhamsi tarehe 28 Mei, 2020 mara baada ya kutembelea Hosteli za Magufuli jijini Dar es Salaam zinazotumiwa na wanafunzi wa UDSM.

Hosteli hizo zilikuwa zikitumika kama karantini kwa watu kukaa hapo kwa siku 14 ili kuangalia kama wana maambukizo ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19).

Matumizi hayo ya hosteli yalifanyika baada ya vyuo kuwa vimefungwa kuanzia tarehe 18 Machi, 2020 kutokana na kuwepo kwa ugonjwa wa corona nchini. Vyuo vyote vitafunguliwa tarehe 1 Juni, 2020.

Katika ziara yake leo, Rais mstaafu Kikwete kabla ya kuwakaribisha wanafunzi, amepokea maelezo kutoka kwa Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Dar es Salaam, Neema Kwemba ambaye alimhakikishia ziko salama.

 

Neema amesema, zaidi ya mwezi sasa hosteli hizo zilikuwa hazitumiki na walifanyan utakasaji wa majengo yote, vyubani, magodoro na kila eneo lote.

Baada ya maekezo hayo, Kikwete akasema, “tunaichukua kauli yenu kwamba pako salama, nataka kuwahakikishia tena vijana, pako salama njooni, kwani tuliowakabidhi wamefanya kama tulivyokubaliana.”

Huku akifurahi, Kikwete akasema, “Basi likitokea la kutokea tutawasiliana, tujue, je wamekuja nao ama wameupatia hapa. Kwa niaba ya chuo kikuu tunawashukuru.”

error: Content is protected !!