April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Prof. Ndalichako atoa ahueni kwa wazazi wa wanafunzi

Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu

Spread the love

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Profesa Joyce Ndalichako, amekemea shule na vyuo nchini humo, kutumia janga la corona kama kitega uchumi kwa kuanzisha michango isiyokubalika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Profesa Ndalichako ametoa onyo hilo leo Alhamisi tarehe 28 Mei, 2020 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari akisisitiza mwongozo wa elimu uliotolewa na wizara ya afya unapaswa kuzingatiwa.

Vyuo vyote na wanafunzi wa kidato cha sita wataanza masomo tarehe 1 Juni, 2020 huku wanafunzi hao wa kidato cha sita wataanza mitihani ya taifa tarehe 29 Mei hadi 16 Juni, 2020.

Vyuo hivyo vinafunguliwa baada ya kufungwa kuanzia tarehe 18 Machi, 2020 baada ya ugonjwa unaosabisishwa na virusi vya corona (COVID-19) kuingia nchini.

Katika mazungumzo yake, Profesa Ndalichako amesema, baada ya kutangaza kufunguliwa kwa vyuo na wanafunzi wa kidato cha sita, kumekuwapo na maelekezo mbalimbali yanayotolewa yanayowachanganya wazazi na walezi.

Amesema, miongoni mwa maelekezo hayo ni michango ambayo haiko kihalali inayowachanganya wanafunzi na wazazi wao.

“Watu waache kutumia corona kama kitega uchumi. Wanafunzi walikwisha kulipa ada lakini shule zilifungwa ghafla. Wanakwenda kuendelea pale walipoishia.”

“Hakuna malipo ya ziada, wasitumie corona kama kitenga uchumi, kuweka michango michango ambayo haina uhalali wowote, tutachukua hatua ikiwamo hata kuzifutia usajili,” amesema Profesa Ndalichako

“Tusiwe na mambo ya kukomoana. Wanafunzi ambao walikuwa hawajakamilisha ada wafanye malipo. Wale waliokuwa wamelipa wanarudi kuendelea na masomo kama walivyoachia ambapo kulikuwa hakuna michango ya ziada,” amesisitiza

Amesema, Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli wakati akitangaza kufunguliwa kwa vyuo na wanafunzi wa kidato cha sita alitoa maekezo kwa wizara ya elimu na ile ya afya kushurikiana ili kuhakikisha tahadhari ya maambukizi inakuwepo.

Waziri huyo amesema, tayari wizara ya afya imekwisha kutoa mwongozo ambao unapaswa kufuatwa na kila mmoja ikiwamo kuwapo kwa maji tiririka ya kunawa pamoja na sababu.

“Shule na vyuo vizingatie mwongozo wa wizara ya afya na siyo kila mmoja anakuja na mwongozo wake. Wengine wanasema, waende na spirit, kiusalama sprit si nzuri na wanafunzi wasienden nayo,” amesema

“Suala la vitaksa mikono ni kama cha ziara, siyo lazima. Vitakasa mikono kama vipo wazingatie hilo. Wizara imekataza kupeleka sprit shuleni, inaweza kutumika kuwasha moto. Marufuku kwenda na spirit shule,” amesema Profesa Ndalichako.

“Watoto wao wawapatie barakoa zilizoshonwa ili aweze kuzifua na kuzipiga pasi mara kwa mara. Wakae mbalimbali mtu na mtu. Unasema mwanafunzi aje na kilo moja ya tangawizi au malimao ya nini, hili koo litabaki salama kweli,” amehoji

error: Content is protected !!