Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Jaji Mwandamizi Pakistan ashangazwa wanapata nini magaidi kutoka kwa nani
Kimataifa

Jaji Mwandamizi Pakistan ashangazwa wanapata nini magaidi kutoka kwa nani

Spread the love

JAJI mwandamizi wa Mahakama ya Juu nchini Pakistani Jaji Qazi Faezi Isa ameshangazwa na  matendo ya Magaidi kwa kushindwa kuelewa wanapata nini kutoka kwa nani. Anaripoti Mwandishi wetu … (endelea).

Akizungumza katika mkutano wa 9 wa mahakama ulioandaliwa na Tume ya Sheria na Haki ya Pakistan katika Jengo la SC Jumamosi, Jaji Isa aliuliza ni ofa gani zinazotolewa kwa ajili ya magaidi.

“Je, tunawaambia ‘tafadhali piga shule tano na sio sita na tafadhali chukua pesa na silaha’,” alisema kwa kejeli, kabla ya kuuliza ni wapi mazungumzo yanafanyika na ni nani aliyeidhinisha.

Jaji Isa alisema kuwa uislam unahimiza kusoma na kwamba aya ya awali iliyoshushwa kwenye Quran ilihimiza elimu inakuaje Magaidi wanakinzana na elimu.

Jaji pia alisikitika kwamba uhakika takwa la  kikatiba wa haki ya kuishi na elimu ya lazima kwa kila mtu umeshambuliwa nchini Pakistan.

“Mazungumzo pekee ambayo Mwislamu wa kweli atakuwa nayo  ni kuwaletea Qurani Tukufu na Sunnah,” alionya, akiongeza kwamba amri ya kwanza ya Mwenyezi Mungu katika Quran Tukufu alikuwa “Iqra” (soma).

Alinukuu data za matukio ya kigaidi ulimwenguni kutoka mwaka 1970 hadi 2019, alisema kulikuwa na mashambulio 1,000 kwenye taasisi za elimu nchini humo.

Jaji Isa pia aligusia masuala kama vile mauaji ya heshima na mabadiliko ya hali ya hewa.

Akiita sheria dhidi ya mauaji ya heshima ‘dead letter,’ alisikitika kuwa sheria ipo lakini haitekelezwi.

“Hii ni moja ya sheria chache ambazo zimetolewa moja kwa moja kutoka kwa Qur’ani Tukufu na inashughulikia kosa la Qazf,” aliongeza.

Aliulizwa kuhusu kurugenzi mpya ya sheria iliyoanzishwa katika Makao Makuu yenye jukumu la kufanya utafiti na kutoa ushauri wa kisheria kuhusu sheria za kimataifa na Katiba.

Katika jibu lake, jaji huyo alisema hafahamu kurugenzi yoyote kama hiyo lakini yuko ‘tayari zaidi’ kutoa ujuzi wake wa Katiba na sheria iwapo ataalikwa. Jukumu la wanawake katika kufanya maamuzi Pakistani

Wakati huo huo, Jaji Mkuu Umar Ata Bandial alivitaka vyombo mbalimbali vya dola kuhakikisha ushirikishwaji wa wanawake katika mchakato wa kufanya maamuzi na akataka juhudi za kutokomeza ukatili wa kijinsia na upendeleo mwingine rasmi na usio rasmi unaowakabili wanawake nyumbani na sehemu za kazi.

Katika hotuba yake ya kuhitimisha mkutano huo, alisisitiza umuhimu wa kufanya mahakama ziwe rahisi kwa wananchi wote, bila kujali jinsia zao, dini, rangi na hali zao kiuchumi.

Alisisitiza matumizi ya teknolojia na kuwataka wadau katika mfumo wa haki ya jinai – polisi na waendesha kuboresha utendaji wao na uratibu wao kwa wao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!