Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko IGP Sirro atuma salamu kwa magaidi wa Msumbiji waliojificha Dar 
Habari Mchanganyiko

IGP Sirro atuma salamu kwa magaidi wa Msumbiji waliojificha Dar 

Spread the love

 

INSPEKTA Jenerali wa Polisi Tanzania , IGP Sirro, amesema wanazifanyia kazi taarifa za uwepo wa watuhumiwa wa vitendo vya  ugaidi waliokimbilia nchini,  wakitokea  Msumbiji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

IGP Sirro ameyasema hayo jana tarehe 10 Septemba 2021, baada ya kurejea nchini akitokea Rwanda alikokwenda kwa ajili ya ziara ya kikazi.

“Lengo la ziara yangu ilikuwa kwenda kufanya tahimini ya kazi tulizokubaliana, kama mnavyokua Mei 2021 IGP wa  Rwanda alikuja nchini, kuna mambo ya msingi tulikubaliana kufanyia kazi pamoja na kupeana taarifa za uhalifu hasa makosa yanayovuka mipaka, dawa za kulevya, ugaidi, usafirishaji binadamu haramu,” alisema  IGP Sirro.

IGP Sirro amesema “tulikubaliana baada ya miezi mitatu tukae tuone tumefanikiwaje, ziara yangu ilikuwa kuona mafanikio na changamoto zilizotokea na tumefanya tathmini wenzetu wana taarifa nzuri kuhusu Msumbiji lakini baadhi ya watu wanashirkiana na Msumbiji wako Dar es Salaam na maeneo mengine, kwa hiyo tutazifanyia kazi.”

Aidha, IGP Sirro alisema katika ziara ya Rwanda amejifunza namna Jeshi la Polisi la nchi hiyo linavyokabiliana na vitendo vya ugaidi na kuahidi kufanyia kazi mikakati yao hapa nchini ili kudhibiti vitendo hivyo.

“Tumeona wenzetu shule za dini, madrasa na sunday school kuna kikosi malaum kupitia kuona mafunzo yanayotolewa je ni ya kizalendo au kuharibu nchi, tumeona ni uzoefu mzuri na sisi tushirkishe viongozi wa dini na timu ya kupambana na makosa ya ugaidi namna gani tupitie  mafunzo ya  kwenye dini shuleni hadi vyuo tuone mafunzo yanayotolewa ni kwa ajili ya kuwajenga au kuwabomoa vinana wa kitanzania,” alisema IGP Sirro.

IGP Sirro alisema “tumeona lingine vijana wanaoharibika hasà waliongia dalili za ugaidi wenzetu wamejenga majumba ya kuwarekebisha na sisi tutaona namna gani tunakuwa na center za namna hiyo, tukipata  vijana wa namna hiyo tunawarekebisha. Tumekubaliana kuona nchi zetu inakuwa shwari.”

“Amani na usalama ni juhudi yetu wote, jambo likiharibika hapa wote tutapata madhara. Jambo la msingi kama ndugu yako, mtu mnakaa mtaa mmoja anaonesha dalili sio nzuri kutoa taarifa. Rwanda walitoa tangazo kama una mtoto humuelewi unatoa taarifa Polisi,” alisema IGP Sorro na kuongeza:

“Nitoe taarifa kama una mke, mume wako una mtoto  amebadilika na unahisi ana makosa ya ugaidi toa taarifa tutakaa naye tumrekebisha awe mtoto mzuri. Tupe taarifa maana kumleta Polisi sio kumshtaki tu, bali kumrekebisha na kuwa mtanzania mzuri.”

1 Comment

  • Sasa umekwenda kwao wakati waliwafukuza magaidi wakimbilie TZ. Hawakuwashinda ndiyo maana wamehamia kwetu.
    Je, nchi ndogo kuliko mkoa mdogo bara ina waislamu wa kuwakaribisha magaidi kwa siku 40 au zaidi?
    Omba jeshi letu lishafishe kama ule mgogoro wa Lindi-Kibiti. Tekeleza haraka kabla hawajawaharibu vijana zaidi. Hamza huenda ni tuna lao.
    Badala ya kuongea sana….chapa kazi tuone umewakamata.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

error: Content is protected !!