Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Michezo Mwili wa Hans Pope kuagwa Dar, kuzikwa Iringa J’tano
Michezo

Mwili wa Hans Pope kuagwa Dar, kuzikwa Iringa J’tano

Marehemu Zacharia HansPope
Spread the love

 

MWILI wa Zacharia Hans Pope, mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa timu ya Simba nchini Tanzania utaagwa kesho Jumatatu, tarehe 13 Septemba 2021, ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hans Pope, ambaye pia alikuwa mjumbe wa kamati ya sharia, hadhi na madaraka ya wachezaji alifariki dunia usiku wa Ijumaa tarehe 10 Septemba 2021, katika Hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam jijini humo alipokuwa akipatiwa matibabu.

Ratiba iliyotolewa na mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara 2020/21, Simba inaonesha mwili wa Hans Pope utazikwa kijijini kwao, Kihesa Mkimbizi mkoani Iringa.

Mbali na kujihusisha na masuala ya michezo, Hans Pope aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili wa Simba aliwahi kuwa Luteni wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), akiwa miongoni mwa waliotaka kufanya jarabio la kumpindua Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, lakini wakashindwa.

Hatua hiyo, ilimfanya Hans Pope na wenzake kutupwa gerezani hadi mwaka 1995 walipokuja kuachiwa na Rais wa wakati huo, Ali Hassan Mwinyi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!